-
Kucheza na moto kwa Trump kunaweza kusababisha mzozo kamili kanda ya Asia Magharibi
Jan 30, 2026 08:30Iran imetangaza kwamba kauli za "kuchochea vita" za Donald Trump zinazidisha mvutano wa kikanda.
-
'Hakuna vita vya masaa 2', yasema Iran ikiapa kutoa jibu la haraka kwa uchokozi wa US au Israel
Jan 30, 2026 04:17Jeshi la Iran limetoa onyo kali kwamba kitendo chochote kipya cha uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kitakabiliwa na jibu kali na la haraka, likisisitiza kwamba uzoefu na tajiriba ya vita vya Juni vimebadilisha kimsingi muelekeo wa kijeshi wa Iran na kanuni zake za makabiliano.
-
Afisa mwandamizi wa jeshi la Israel: Iran ni dola moja kuu kwa makombora duniani
Jan 30, 2026 04:17Kamanda wa zamani wa mitambo ya ulinzi wa anga wa utawala wa kizayuni wa Israel ameielezea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni moja ya madola makuu duniani kwa upande wa masuala ya anga na ulimwengu wa makombora, na akasema, Tehran itailenga Tel Aviv iwapo kutakuwa na shambulio lolote litakalofanywa na Marekani dhidi yake.
-
Qalibaf: Iran haipingi mazungumzo, inataka diplomasia ichukue mkondo wake
Jan 29, 2026 23:42Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa Tehran haipingi msingi wa mazungumzo na diplomasia ambao lazima uwe wa aina yake na wenye mlingano kwa mujibu wa kuheshimiana pande mbili.
-
'Ni rahisi - Trump ameshindwa': Wanamtandao wakosoa vitisho vya kijeshi vya Marekani dhidi ya Iran
Jan 29, 2026 09:35Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekosoa vitisho vya kijeshi vya mara kwa mara vya Rais wa Marekani, Donald Trump dhidi ya Iran, ambapo hivi karibuni alitishia Iran kwa kisingizio cha miradi ya nyuklia ya nchi hiyo. Wamesema kuwa Israel inaiburuta Washington katika vita vingine kwa niaba ya serikali ya Tel Aviv.
-
Nujaba kwa maadui wa Iran: Vita vinaweza kufika milangoni kwenu
Jan 29, 2026 02:57Katibu Mkuu wa kundi la kupambana na ugaidi la Harakat al-Nujaba la Iraq amewaonya vikali maadui wa Iran kuhusu matokeo mabaya ya uchokozi wowote mpya ambao wanaweza kufanya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Araghchi: Mazungumzo hayawezi kufanikiwa chini ya vitisho
Jan 29, 2026 00:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi ameonya kwamba, kutwisha diplomasia kupitia vitisho vya kijeshi hakuwezi kuwa na ufanisi au tija, akisema kwamba hakuna uamuzi wowote ambao umefanywa na Tehran kufikia juu ya kufanya mazungumzo na Marekani.
-
Iran: Maadui wajiandae kwa 'jibu la uharibifu' wakituchokoza
Jan 29, 2026 00:18Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Iran ameonya kwamba, hatua yoyote ghalati dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu itawasababishia maadui uharibifu mkubwa, akisisitiza kwamba vitisho dhidi ya Tehran kupitia maonyesho ya kijeshi havilishughulisha taifa hili.
-
Mtaalamu wa kijeshi: Utitiri wa droni za Iran ni 'tishio halisi' kwa vyombo vya majini vya Marekani
Jan 28, 2026 07:02Mtaalamu wa kijeshi wa ndege zisizo na rubani ameonya kuwa, utitiri wa ndege zisizo na rubani za Iran ni "tishio halisi" kwa vyombo vya jeshi la wanamaji la Marekani vyenye thamani kubwa, wakati huu ambapo Washington inaripotiwa kuwa inaendelea kujizatiti kijeshi katika eneo la Asia Magharibi.
-
Iran ilivyofanikiwa kuvunja mtandao wa mawasiliano ya kigaidi kwa kukata intaneti
Jan 28, 2026 04:30Iran ilifanikiwa kuvuruga na hatimaye kuvunja mtandao wa mawasiliano wa makundi ya kigaidi na washirika wao wa nje kwa hatua ya kukata intaneti wakati wa machafuko ya Januari 2026.