-
Iran yakaribisha mkutano wa makundi ya Wapalestina huko Beirut
Sep 05, 2020 06:45Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kikao cha pamoja cha makundi ya Wapalestina kilichofanyika katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut ni ishara kwamba viongozi wa Palestina wapo macho na wamesimama kidete mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na washirika wake.
-
Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya sekta ya Petrokemikali ya Iran, kielelezo cha kuishiwa na kupumbaa Washington
Sep 04, 2020 06:52Katika hatua za kutaka kuiburuza na kuilazimisha Iran isalimu amri kwa matakwa yake haramu na ya kinyume cha sheria, Serikali ya Trump iliamua kuanzisha vita vya mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu; na baada ya kujitoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mnamo mwezi Mei 2018, ilianza kuiwekea Tehran vikwazo vikali zaidi kuwahi kushuhudiwa.
-
Iran yalijia juu jarida la Ufaransa kwa kumtusi Mtume Muhammad (saw)
Sep 04, 2020 02:56Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW).
-
"Vipigo dhidi ya Marekani katika Baraza la Usalama vimetokana na kusimama kidete Wairani"
Sep 03, 2020 22:12Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushindwa mtawalia njama za Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumetokana na kusimama kidete taifa hili.
-
Iran: Makombora yetu yana uwezo na muundo wa kipekee
Sep 02, 2020 03:32Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema makombora yaliyozalishwa hapa nchini yana muundo wa aina yake na uwezo wa kipekee, jambo ambalo limeimarisha uwezo wa kujihami taifa hili.
-
Araqchi: Wanachama wa JCPOA hawaitambui Marekani kama mshirika wao
Sep 01, 2020 23:01Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema nchi zilizosalia katika makubaliano ya nyuklia ya Iran haziitambui Marekani kuwa mwanachama au mshirika wa mapatano hayo ya kimataifa.
-
Rais Rouhani: Mitazamo ya Iran na Niger katika masuala ya kimataifa inafanana
Sep 01, 2020 03:18Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo yake ya simu na mwenzake wa Niger kuwa nchi mbili hizi zimekuwa na ushirikiano amilifu na mitazamo inayofanana katika masuala na taasisi za kimataifa na kubainisha kuwa, nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika bila shaka itakabiliana na uchukuaji wa maamuzi ya upande mmoja wa Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Iran: Marekani haina haki wala kibali cha kutumia "Snapnack Mechanism"
Sep 01, 2020 03:16Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Marekani haina haki, idhini wala kibali cha kutumia utaratibu wa kurejesha upya vikwazo ilivyokuwa imewekewa Iran huko nyuma na UN unaofahamika kama 'Snapback Mechanism."
-
Iran: Magaidi wa MKO wanapewa hifadhi na US na EU licha ya kuua maelfu ya Wairani
Aug 30, 2020 06:32Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema nchi za Ulaya na Marekani zinawapa hifadhi wanachama wa kundi la kigaidi la Munafikin (MKO) licha ya genge hilo kuua kikatili maelfu ya Wairani.
-
Umbumbumbu wa Marekani katika masuala ya sheria, wameshindwa na sasa wanatoa vitisho
Aug 29, 2020 05:48Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amekosoa jitihada zinazofanywa na Marekani kwa ajili ya kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran kuanzia tarehe 20 Oktoba mwaka huu wa 2020 na kusema: Viongozi wa serikali ya Marekani ni mbumbumbu katika masuala ya sheria na hawajui lolote kuhusiana na tendaji wa Umoja wa Mataifa.