-
Trump atafakari pendekezo la mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Iran
Apr 02, 2025 23:05Ikulu ya Marekani White House inatathmini pendekezo la kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Iran; na wakati huo huo inaongeza kiwango cha vikosi vya jeshi lake vamizi katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) ili kujiandaa kwa operesheni tarajiwa za kijeshi dhidi ya Tehran.
-
"Saudia, UAE, Qatar, Kuwait zapiga marufuku ndege za US kufanya mashambulio"
Apr 02, 2025 23:04Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba ya Uajemi yamepiga marufuku ndege za kivita za Marekani kutumia viwanja vyake vya ndege au anga zao kufanya mashambulizi dhidi ya Yemen.
-
Jumatano, tarehe Pili Aprili, 2025
Apr 01, 2025 22:56Leo ni Jumatano tarehe 3 Shawwal 1446 Hijria sawa na Aprili Pili mwaka 2025.
-
Araghchi: Maadui watajuta kwa kutoa vitisho dhidi ya Iran
Apr 01, 2025 08:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitamruhusu mtu yeyote kuzungumza nayo kwa lugha ya ubabe na vitisho, akiwaonya maadui kwamba watajuta kulitishia taifa hili.
-
Wizara ya Ulinzi ya Iran: Chokochoko dhidi yetu zitakabiliwa na jibu madhubuti
Apr 01, 2025 07:23Wizara ya Ulinzi ya Iran imewaonya vikali maadui kwamba, kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya taifa hili kitakabiliwa na jibu la haraka na madhubuti.
-
Baqaei: Marekani ijitayarishe kwa athari za hatua yoyote dhidi ya Iran
Mar 31, 2025 08:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametangaza katika ujumbe wake kwamba, tishio lolote la rais wa nchi la kuishambulia Iran kwa mabomu ni ukiukaji wa wazi na kiini cha amani na usalama wa kimataifa.
-
Kamanda: Iran ina uwezo wa kupiga ngome za adui popote pale
Mar 30, 2025 03:58Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Admeli Alireza Tangsiri amesema kwa mara nyingine tena kuwa, uwezo wa kijeshi wa Iran ni wa kipekee, huku akionya dhidi ya vitisho akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haiwezi kufanya mazungumzo na yeyote kuhusu maghala yake ya makombora.
-
Hizbullah: Iran ndiye muungaji mkono mkuu wa kadhia ya Palestina
Mar 30, 2025 03:51Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza nafasi muhimu ya Iran katika kuunga mkono kadhia ya Palestina ya kukombolewa kuondokana na uchokozi na uvamizi wa Israel huku akiulaani vikali utawala wa Israel kwa ukatili wake katika eneo zima ambao unawezeshwa kwa kiasi kikubwa na uungaji mkono wa Marekani.
-
China: Tuko tayari kustawisha uhusiano wa kijeshi na Iran na Russia
Mar 29, 2025 23:08Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China amezungumzia mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyofanywa na majeshi ya Wanamaji ya nchi hiyo, Iran na Russia na kusisitiza kuwa Beijing iko tayari kustawisha ushirikiano wa kijeshi na nchi hizo mbili.
-
Mamilioni ya Wairani washiriki maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Mar 28, 2025 04:15Wananchi Waislamu wa Iran kote nchini wamejitokeza kwa mamilioni kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, kuonyesha mshikamano na Palestina, na kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.