-
Mamilioni wamuaga Kiongozi Shahidi Ayatullah Khamenei katika miji ya Najaf na Karbala nchini Iraq
Jul 08, 2026 14:19Mamilioni ya waombolezaji leo Jumatano walikusanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq kwa ajili ya kuaga na kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na familia yake waliouliwa shahidi katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
-
Wairaqi wasubiri kwa hamu kupokea mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Jul 07, 2026 04:34Wakati ukikaribia kwa ajili ya kufanyika mazishi ya mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika miji ya Najaf Ashraf na Karbala Mualla, Iraq inashuhudia maandalizi makubwa yasiyokuwa ya kawaida yanayohusisha serikali, wananchi, viongozi wa makabila, vikosi vya usalama na taasisi za huduma.
-
Iraq yachora mstari mwekundu; yasema: Ardhi ya nchi hiyo haitatumika kufanya mashambulizi dhidi ya Iran au nchi jirani
May 18, 2026 04:33Iraq imetangaza wazi kuwa kamwe haitaruhusu ardhi yake itumike kwa ajili ya kufanya mashambulizi dhidi ya nchi jirani, hasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iraq yamueleza mjumbe wa Marekani: Uundaji wa serikali ni 'suala letu la ndani'
Feb 24, 2026 08:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein amesema, uundaji wa serikali mpya ya nchi hiyo ni "suala la ndani," ukiwa ni mjibizo uliotolewa wiki chache baada ya Marekani kutishia kufuta msaada na uungaji mkono wake kwa nchi hiyo ya Asia Magharibi.
-
Maelfu ya Wairaqi wajiandikisha kuingia vitani kuisaidia Iran endapo itashambuliwa na Marekani
Feb 08, 2026 02:46Maelfu ya Wairaqi wamesaini hati ya ahadi ya kusaidia kuihami Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iwapo itashambuliwa kijeshi na Marekani.
-
Nujaba kwa maadui wa Iran: Vita vinaweza kufika milangoni kwenu
Jan 29, 2026 02:57Katibu Mkuu wa kundi la kupambana na ugaidi la Harakat al-Nujaba la Iraq amewaonya vikali maadui wa Iran kuhusu matokeo mabaya ya uchokozi wowote mpya ambao wanaweza kufanya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Trump atishia kuikatia misaada Iraq endapo Nouri al-Maliki atakuwa Waziri Mkuu
Jan 28, 2026 06:58Rais wa Marekani Donald Trump amedai katika ujumbe unaoakisi uingiliaji wa wazi wa masuala ya ndani ya Iraq kwamba Nouri al-Maliki hapasi kuwa waziri mkuu, kwa sababu kama atachaguliwa kushika wadhifa huo, Marekani haitatoa tena misaada kwa nchi hiyo.
-
Kata'ib Hizbullah yatoa wito kwa wanamuqawama kujiandaa kwa 'vita' ili kuinga mkono Iran
Jan 26, 2026 03:06Harakati ya Kata’ib Hizbullah ya Iraq (Brigedi za Hizbullah) imetangaza kuwa iko tayari kushiriki katika vita vyovyote vitakavyotokea ili kuilinda Iran, ikitoa wito kwa wanamapambano duniani kote kujiandaa kwa ajili ya hilo.
-
Wairaqi waunga mkono Hizbullah na Ansarullah baada ya tangazo la kuzuiliwa mali zao kimakosa
Dec 05, 2025 04:21Mitaa ya mji mkuu wa Iraq, Baghdad usiku wa kuamkia leo ilishuhudia misafara mirefu ya magari, yaliyokuwa yakipeperusha bendera za harakati za Muqawama wa Kiislamu za Hizbullah ya Lebanon na Ansarullah ya Yemen, na kutangaza mshikamano wa umma na harakati hizo za Muqawama dhidi ya vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Al-Sudani asema, ataanza kufanya mazungumzo ya kuunda serikali mpya ya Iraq
Nov 13, 2025 08:55Waziri Mkuu wa Iraq Mohammad Shia al-Sudani amesema, ataanza kufanya mazungumzo hivi karibuni kwa ajili ya kuunda serikali mpya wakati muungano wake unaonekana kuongoza katika uchaguzi wa bunge.