-
Hashdu Sha'abi Iraq: Tupo tayari kwenda kuisafisha Syria kutokana na Daesh
May 30, 2017 03:57Msemaji wa Harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi nchini Iraq, ameelezea utayarifu wa wapiganaji wake kwa ajili ya kupambana na genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh ndani ya ardhi ya Syria kupitia ushirikiano kamili wa serikali ya nchi hiyo.
-
Kiongozi wa Mayazidi Iraq, awataka vijana wa kabila hilo kujiunga na Hashdu Sha'abi
May 29, 2017 09:39Kiongozi Mkuu wa watu wa kabila la Mayazidi nchini Iraq, sambamba na kutoa pongezi na shukurani za dhati kwa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi nchini, amewataka pia vijana wa kabila hilo kujiunga na harakati hiyo kuilinda nchi.
-
Jaafari: Iraq haitounga mkono muungano dhidi ya Iran
May 28, 2017 23:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq amesema nchi yake katu haitounga mkono wala kushirikiana na muungano wowote uliopo au utakaoundwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Vikosi vya ulinzi vya Iraq katika hatari ya mashambulizi ya Marekani
May 24, 2017 23:03Katika hali ambayo harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi nchini Iraq katika kukabiliana na ugaidi inaendelea kupongezwa na viongozi, wananchi na hata katika fikra za walio wengi, wanamapambano wa harakati hiyo bado wanaendelea kushambuliwa na ndege za kijeshi za Marekani.
-
Muqtada Sadr aitisha maandamano nje ya ubalozi wa Bahrain, Baghdad
May 24, 2017 03:23Sayyid Muqtada Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Sadr ya Iraq amewataka wananchi wa taifa hilo la Kiarabu wakusanyike nje ya ubalozi wa Bahrain mjini Baghdad, kulalamikia ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Aal-Khalifa dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na viongozi wao nchini humo.
-
Onyo la Waziri Mkuu wa Iraq juu ya njama za kimataifa dhidi ya taifa hilo
May 20, 2017 23:25Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mjini Baghdad hapo siku ya Ijumaa Haider al-Abad, Waziri Mkuu wa lraq alikosoa vikali hatua ya kufanyika mwezi mmoja uliopita vikao vya eti kujadili mustakbali wa lraq huko mjini Geneva Uswisi kwa ubunifu wa Marekani na vilevile mjini lstanbul kwa ubunifu wa Uturuki.
-
Vita laini nchini Iraq baada ya kukombolewa mji wa Mosul kutoka kwa magaidi wa ISIS
May 18, 2017 02:40Sayyid Ammar al-Hakim, Mkuu wa Muungano wa Kitaifa nchini Iraq, amesema kuwa, baada ya kukombolewa mji wa Mosul, sasa maadui wanakusudia kuanzisha vita laini vyenye lengo la kuibua tofauti baina ya taifa la Iraq.
-
90% ya mji wa Mosul wakombolewa, Magaidi 170 wauawa Iraq
May 16, 2017 09:56Kamanda wa Operesheni ya Jeshi la Iraq ametangaza habari ya kukombolewa asilimia 90 ya maeneo ya magharibi mwa mji wa Mosul yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
-
Magaidi zaidi ya 140 wa Daesh waangamizwa Mosul, Iraq
May 15, 2017 01:10Kamanda wa Polisi Kuu ya Iraq ametangaza kuwa zaidi ya magaid 140 wa kundi la ukufurishaji la Daesh (ISIS) wameangamizwa katika eneo la Al-Haramat magharibi mwa mji wa Mosul.
-
Independent : Daesh (ISIS) linawatesa kwa njaa watoto wa Kiiraqi ili kuwashajiisha wajiripue
May 12, 2017 11:44Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) linawatesa kwa njaa watoto wadogo wa Iraq kwa ajili ya kuwalazimisha watekeleze vitendo vya kigaidi vya kujiripua katika maeneo ya raia wa kawaida.