-
Ansarullah: Saudia na Imarati zinashirikiana na Israel dhidi ya Waislamu
Jun 19, 2020 23:33Kiongozi wa harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah amezionya vikali Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu dhidi ya kuendeleza njama za kutaka kuufanya wa kawaida uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kwamba, Riyadh na Abu Dhabi zinashirikiana na Tel Aviv ambayo inajulikana ni adui mkubwa wa ulimwengu wa Kiislamu.
-
Jeshi la Lebanon lajiweka sawa baada ya askari wa Israel kwenda mpakani
Jun 19, 2020 23:27Jeshi la Lebanon limejiweka katika hali ya tahadhari baada ya kuripotiwa uwepo wa makumi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mpaka wa nchi hiyo ya Kiarabu na Palestina.
-
Israel kujenga 'vitongoji 300 vya Trump' katika Milima ya Golan, Syria
Jun 15, 2020 02:23Utawala ghasibu wa Israel unapanga kujenga mamia ya vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika Miinuko ya Golan nchini Syria, vitakavyoitwa "Miinuko ya Trump".
-
Hamas yataka wanazuoni wa Kiislamu waunde kamati ya kuzima njama za Israel
Jun 14, 2020 22:41Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametoa mwito kwa wanazuoni wa Kiislamu kuunda kamati ya uratibu itakayopewa jukumu la kuunda na kutekeleza mpango wa kistratajia wa kuunga mkono kadhia ya Palestina na kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel na Rais Donald Trump wa Marekani zilizopewa jina la "Muamala wa Karne."
-
Waziri wa zamani wa Misri: Israel ni adui wa kiistratajia wa Wamisri
Jun 07, 2020 22:08Waziri wa zamani wa Misri ameutaja utawala wa Kizayuni wa Israel kama adui wa kistratajia wa wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika.
-
Tamim: Wakati umefika wa kuweka wazi uhusiano wa Israel na Waarabu
Jun 07, 2020 22:05Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi la Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu ameibua mijadala na wimbi la malalamiko baada ya kutoa mwito kwa nchi za Kiarabu kuufanya wa kawaida uhusiano wao na utawala haramu wa Israel.
-
Hamas yalaani mashambulizi ya Israel nchini Syria
Jun 05, 2020 03:26Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amelaani mashambulizi ya makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Syria.
-
Jihad Islami: Tawala za Israel na Marekani ni za kibaguzi na kigaidi
Jun 01, 2020 21:56Mjumbe wa Idara ya Siasa ya harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema kuwa, Marekani na utawala haramu wa Israel ni tawala za kibaguzi na kigaidi ambazo zilianzishwa kwa msingi wa kuvamia, kuua, kufanya ubaguzi na kuwanyonya wanadamu.
-
Familia: Mpalestina aliyeuawa na jeshi la Israel alikuwa mlemavu
May 31, 2020 06:58Kijana wa Kipalestina aliyeuawa jana Jumamosi na wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kupigwa risasi katika mji mtakatifu wa Quds alikuwa mlemavu.
-
Sayyid Nasrullah: Utawala wa kibaguzi wa Israel utaangamia
May 27, 2020 03:31Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Kizayuni wa Israel utasambaratika na kuangamia na kwamba matukio yote yanayoshuhudiwa hivi sasa katika eneo la Asia Magharibi yapo dhidi ya maslahi ya utawala huo pandikizi.