-
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu vita vya Gaza; athari za kutisha za jinai za Israel
Nov 27, 2025 10:17Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imefichua vipengele vipya vya athari za kutisha za vita vya Gaza. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa vita vya utawala wa Kizayuni huko Gaza vimeunda shimo la kutisha na kwamba ujenzi mpya wa ukanda huu utahitaji kwa uchache dola bilioni 70 na muda wa miongo kadhaa, takwimu zinazodhihirisha wazi kina cha janga hili.
-
Haaretz: Netanyahu amepelekea Israel kushindwa katika pande zote, hususan dhidi ya Iran
Nov 26, 2025 12:18"Sera za waziri mkuu Benjamin Netanyahu zimepelekea kushindwa Israel katika pande zote za kidiplomasia, kijeshi, na kimkakati, hususan dhidi ya Iran". Hayo ni kwa mujibu wa Haaretz, gazeti la Israel linalochapishwa kwa lugha ya Kiebrania.
-
Mvutano mkali ulitawala mazungumzo ya Trump na Bin Salman kuhusu kuanzisha uhusiano na Israel
Nov 26, 2025 11:44Duru zenye taarifa zimedokeza kuwa, mkutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman uliofanyika wiki iliyopita katika Ikulu wa White House ulishuhudia mvutano wa dhahiri kwa sababu Trump aliishinikiza Riyadh ijiunge na Mkataba wa Abraham, wa kuanzisha uhusiano rasmi na utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Caracas yamhutubu waziri wa Israel: Jina Venezuela ni kubwa, haliwezi kutamkwa na kinywa chako kichafu
Nov 26, 2025 03:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela ametumia lugha kali kujibu tuhuma za waziri wa mambo ya nje wa utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Caracas, kwa kumwita waziri huyo "mhalifu wa kivita" ambaye iwe sasa hivi au baadaye lazima akawajibishwe mbele ya vyombo vya haki na sheria vya kimataifa.
-
Kwa nini mkataba wa gesi kati ya Israel na Misri unakaribia kusambaratika?
Nov 25, 2025 10:22Hitilafu za kisiasa na kiusalama kati ya utawala ghasibu wa Israel na Misri zimechukua zimefikia katika uga wa kiuchumi, na sasa zimefikisha mkataba mkubwa zaidi wa gesi kati ya Tel Aviv na Cairo kwenye ukingo wa kusambaratika.
-
Marekani yabatilisha viza ya waziri wa zamani wa Afrika Kusini aliyefanikisha kesi ya ICJ dhidi ya Israel
Nov 23, 2025 07:01Marekani imefuta viza ya waziri wa zamani wa Mahusiano ya Kimataifa wa Afrika Kusini Naledi Pandor mapema wiki hii, katika kile kinachoonekana kama hatua za hivi karibuni za Washington za kuiadhibu Pretoria kwa sababu kuuburuza utawala wa kizayuni wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa mauaji ya kimbari uliyofanya dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.
-
Sababu za Ripota wa UN za kuonya kuhusu kuendelea Ulaya kuipa silaha Israel
Nov 22, 2025 02:24Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuendelea nchi za Ulaya kuisheheneza silaha Israel licha ya kwamba kuna ushahidi wa kutosha na usiopingika wa jinsi utawala wa Kizayuni unavyotumia silaha hizo kufanya jinai na mauaji ya umati dhidi ya watu wasio na hatia.
-
Israel yafanya mashambulio ya kinyama Ghaza, yaua Wapalestina 28 na kujeruhi 77
Nov 20, 2025 06:09Wapalestina wasiopunguua 28 wameuawa shahidi katika wimbi jipya la mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza, yakiwa ni moja ya ukiukaji mkubwa zaidi wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani na kuanza kutekelezwa mwezi uliopita wa Oktoba.
-
Kwa nini hati ya makubaliano ya kijeshi kati ya India na utawala wa Kizayuni ni hatua ya kuleta ukosefu wa utulivu Asia?
Nov 20, 2025 02:53India na utawala wa Kizayuni wa Israel zimepanua ushirikiano wao wa kijeshi na kiviwanda kwa kutiliana saini hati mpya ya maelewano na ushirikiano.
-
Kampuni ya silaha ya Israel ya Elbit imeingiza mapato makubwa wakati wa mauaji ya kimbari ya Gaza
Nov 19, 2025 12:30Kampuni ya Israel inayoongoza kwa utengenezaji wa silaha, Elbit Systems, imetangaza ongezeko kubwa la faida iliyopatikana katika muda wa robo mwaka kufuatia miezi kadhaa ya ushiriki wa kampuni hiyo katika mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza kupitia utoaji silaha, zana za kijeshi na mifumo ya ufuatiliaji, huku ikipata mikataba mipya barani Ulaya.