-
Dehqan: Juhudi za Israel za kuunda muungano dhidi ya Iran zitafeli
Feb 22, 2017 00:36Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema juhudi za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuunda muungano dhidi ya Iran hazitafua dafu.
-
Qassemi: Kufanana misimamo ya Israel na Saudia sio jambo la ghafla
Feb 20, 2017 03:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kufanana misimamo hasi dhidi ya Iran ya Kiislamu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia na Waziri wa Vita wa Israel katika kikao cha Usalama cha mjini Munich, Ujerumani sio jambo la ghafla.
-
Kufichuliwa kikao cha siri kati ya Waarabu na Wazayuni katika bandari ya Aqaba
Feb 19, 2017 23:21Gazeti moja la Kizayuni limefichua kufanyika kikao cha siri mwaka jana kati ya Marekani, utawala wa Kizayuni, Jordan na Misri katika bandari ya Aqaba huko Jordan kwa ajili ya kuchunguza mazungumzo ya mapatano na upande wa Palestina.
-
Lebanon: Hatua yoyote ya kichokozi ya Israel itapata jibu kali
Feb 19, 2017 03:05Rais Michel Aoun wa Lebanon ameonya kuwa, iwapo utawala haramu wa Israel utachukua hatua yoyote ya kukanyaga uhuru wa kujitawala nchi hiyo ya Kiarabu, basi ujiandae kwa jibu kali.
-
Abbas afanya mazungumzo na spika wa zamani wa Knesset
Feb 18, 2017 04:49Rais wa serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekutana na kufanya mazungumzo na spika wa zamani wa Bunge la Israel, Knesset katika mji wa Ramallah siku chache tu baada ya Waziri wa Utamaduni wa utawala huo haramu kutoa wito wa kufutwa kikamilifu Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) katika Ukanda wa Gaza.
-
Ismail Hania: Vita vya Palestina na Israel ni kuhusu Masjidul Aqswa
Feb 18, 2017 04:14Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, vita vya Palestina na utawala wa Kizayuni vinahusiana na Msikiti wa al Aqsa na utambulisho wa Palestina.
-
Imam wa msikiti wa Al-Aqsa: Hatutotekeleza sheria ya marufuku ya Adhana
Feb 14, 2017 04:13Sheikh Ikrima Sabri, Khatibu na Imam wa msikiti wa Al-Aqsa amesema sheria ya kupiga marufuku sauti ya adhana katika misikiti ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni ya kidhalimu na kusisitiza kwa kusema: Sitatekeleza uamuzi huo.
-
Tahadhari kuhusu njama za Marekani na Israel za kuibua mifarakano baina ya Waislamu
Feb 13, 2017 23:44Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema: "Maadui wa Uislamu hasa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel wanatumia uwezo wao wote kuibua mifarakano katika ulimwengu wa Kiislamu."
-
Spika wa Bunge la Kuwait ataka Israel ifukuzwe kwenye Umoja wa Mabunge
Feb 13, 2017 00:50Kuwait imelaani ujenzi wa vitongoji vya walowezi unaofanywa na utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kutoa wito wa kutaka utawala huo ufukuzwe katika Umoja wa Kimataifa wa Mabunge.
-
Avigdor Lieberman: Wapalestina wote waondoke Israel!
Feb 12, 2017 04:01Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel amewataka Wapalestina wote waondoke mara moja katika ardhi zao zilizoghusubiwa na utawala huo bandia.