Avigdor Lieberman: Wapalestina wote waondoke Israel!
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25035-avigdor_lieberman_wapalestina_wote_waondoke_israel!
Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel amewataka Wapalestina wote waondoke mara moja katika ardhi zao zilizoghusubiwa na utawala huo bandia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 12, 2017 04:01 UTC
  • Avigdor Lieberman: Wapalestina wote waondoke Israel!

Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel amewataka Wapalestina wote waondoke mara moja katika ardhi zao zilizoghusubiwa na utawala huo bandia.

Akiongea hapo jana katika Kanali ya 2 ya Israel, Avigdor Lieberman alisema Wapestina wanaoishi katika eti miji ya Israel wanafaa kufurushwa na walazimishwe kwenda Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wakaishi chini ya uongozi wa Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.

Akitumia maneno makali na ya kejeli, Liberman ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel amesema: "Nyinyi ni Wapalestina, mnapaswa kwenda kwa Abu Mazen (Mahmoud Abbas), atakulipeni marupurupu ya kutofanya kazi na ashughulikie masuala yenu ya afya na matibabu yenu."

Ameongeza kuwa, utawala huo ghasibu unashauriana na Marekani kuhusu mpango wa 'kuudhibiti kikamilifu' Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Ujenzi wa vitongoji vya walowezi za Kiyahudi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu

Lieberman amekuwa akitoa matamshi makali na ya chuki dhidi ya Wapalestina mara kwa mara. Febuari mwaka jana, alitoa wito kwa  jeshi la utawala huo bandia kuhakikisha kwamba linamuua Ismail Haniya, afisa wa ngazi za juu wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).

Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuutaka utawala huo bandia usitishe ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu, kwa kiburi kamati ya ujenzi wa vitongoji ya utawala wa Kizayuni wa Israel ilipitisha uamuzi wa kujengwa nyumba nyingine mpya 181 katika mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu.