Qassemi: Kufanana misimamo ya Israel na Saudia sio jambo la ghafla
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25384-qassemi_kufanana_misimamo_ya_israel_na_saudia_sio_jambo_la_ghafla
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kufanana misimamo hasi dhidi ya Iran ya Kiislamu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia na Waziri wa Vita wa Israel katika kikao cha Usalama cha mjini Munich, Ujerumani sio jambo la ghafla.
(last modified 2026-04-23T06:05:17+00:00 )
Feb 20, 2017 03:55 UTC
  • Qassemi: Kufanana misimamo ya Israel na Saudia sio jambo la ghafla

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kufanana misimamo hasi dhidi ya Iran ya Kiislamu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia na Waziri wa Vita wa Israel katika kikao cha Usalama cha mjini Munich, Ujerumani sio jambo la ghafla.

Bahram Qassemi amesema kuwa ushahidi unaonyesha kuwepo urafiki na ushirikiano wa karibu sana baina ya tawala hizo kuhusiana na masuala mengi ya Mashariki ya Kati. Amesema kuwa, kufuatia kushindwa mtawalia tawala hizo katika eneo hili, sasa zimeamua kuchochea hisisa za watu duniani dhidi ya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia

Aidha Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kukaririwa tuhuma bandia na zenye kuchekesha kunakofanywa na Saudia ambayo ndio chimbuko na muungaji mkono mkuu wa kundi la kigaidi la Daesh, kamwe hakuwezi kuficha hata kidogo ushirikiano wa kiimani, kimafunzo, kifedha na kiintelejensia uliopo baina ya utawala wa Saudi Arabia na makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakitekeleza jinai dhidi ya watu wasio na hatia katika nchi za eneo hili na duniani kwa ujumla.

Picha muhimu iliyoonyeshwa na kanali za Israel ikimuonyesha Netanyahu akiwajulia hali magaidi wa ISIS waliokuwa wakipatiwa matibabu Israel

Jumapili ya jana Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa Utawala wa Kizayuni na Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia walitoa matamshi ya pamoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo sanjari na kukosoa vikali makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 walidai kuwa Tehran ni muungaji mkono wa ugaidi. Matamshi ya mawaziri hao wa Israel na Saudia yalitolewa katika hali ambayo tawala hizo yaani Saudi Arabia na utawala haramu wa Kizayuni, zimekuwa zikishirikiana bega kwa bega na makundi ya kigaidi yanayotekeleza jinai nchini Syria, Iraq na Yemen. Mbali na Saudia na Israel kuwasaidia magaidi kifedha na kisilaha, Tel-Aviv imekuwa ikiwasaidia kimatibabu huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu magaidi waliojeruhiwa.