-
Serikali ya Israel yagawanyika kuhusu mjibizo wa kutoa kwa nchi za Magharibi zilizoitambua nchi ya Palestina
Sep 22, 2025 23:29Chaneli ya 12 ya televisheni ya utawala wa kizayuni wa Israel imeripoti kuwa, mizozo ndani ya baraza la mawaziri la utawala huo inazidi kuongezeka baada ya mawaziri muhimu kutojumuishwa katika mijadala nyeti kuhusu jinsi ya kutoa mjibizo dhidi ya hatua ya karibuni ya nchi za Magharibi ya kuitambua nchi ya Palestina.
-
Rais wa Baraza la EU: Lengo hasa la Israel ni kuufanya uundwaji wa nchi ya Palestina usiwezekane
Sep 22, 2025 23:27Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa amesema hatua za kijeshi zinazochukuliwa na Israel huko Ghaza si suala tena la kujilinda na zinaonekana kuwa na lengo la kuufanya uundaji wa nchi ya Palestina hapo baadaye usiwezekane.
-
Kwa nini Tel Aviv inaogopa kutambuliwa rasmi nchi huru ya Palestina?
Sep 22, 2025 07:50Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limejiweka kwenye hali ya tahadhari kukabiliana na matukio yanayoweza kutokea baada ya baadhi ya nchi za Magharibi kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina.
-
Amnesty International imetaka Israel iwekewe vikwazo haraka iwezekanavyo
Sep 21, 2025 07:33Shirika la Amnesty International limeitaka jamii ya kimataifa kuiwekea Israel vikwazo haraka iwezekanavyo kutokana na vita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kutekelezwa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
-
Je, Israel inakabiliwa na "Hatima ya Afrika Kusini"?
Sep 21, 2025 02:33Tovuti ya Kiingereza ya BBC katikati ya Septemba 2025 katika makala ya kina yenye kichwa cha habari kilichosomeka "Je, Israel Inakabiliwa na 'Hatima ya Afrika Kusini'?" Ilizungumzia suala la kujikariri uzoefu wa Afrika Kusini kwa utawala ghasibu wa Israel.
-
Je, upo uwezekano wa kutokea vita kati ya Uturuki na utawala wa Kizayuni?
Sep 20, 2025 06:19Mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Qatar yamezidisha mivutano kati ya Uturuki na Israel na kuibua uwezekano wa kutokea makabiliano ya moja kwa moja kati ya Ankara na Tel Aviv.
-
Baada ya kuangamizwa askari 6 wa kizayuni, HAMAS yaionya Israel: Ghaza itageuka 'kaburi' la askari wenu
Sep 19, 2025 07:38Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala wa kizayuni wa Israel kwamba hatua yake ya kuzidi kujiingiza ndani ya Mji wa Ghaza kutaugeuza mji huo kuwa "kaburi," la wanajeshi wa kizayuni baada ya sita miongoni mwao kuangamizwa na wanamuqawama wa Palestina katika matukio tofauti wakati wa jeshi la Israel likiwa linaendeleza mashambulizi makali na ya kinyama yanayolenga kulikalia kwa mabavu eneo lote la Ghaza.
-
UNIFIL yaitaka Israel ikomeshe mashambulizi, iondoke kikamilifu katika ardhi ya Lebanon
Sep 19, 2025 07:34Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon, UNIFIL imesema, shambulio la anga lililofanywa na jeshi la Israel jana usiku kusini mwa Lebanon ni ukiukaji wa wazi wa azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama na tishio la moja kwa moja kwa hali tete ya uthabiti katika eneo hilo.
-
Askari wanne wa utawala wa kizayuni waangamizwa, wanane wajeruhiwa kusini mwa Ghaza
Sep 18, 2025 07:12Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa wanajeshi wanne wa utawala wa kizayuni wa Israel wameangamizwa na wengine wanane wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu lililotegwa ardhini kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
-
Balozi wa Marekani Israel: Israel ndiye mshirika wetu pekee wa kweli katika eneo la Mashariki ya Kati
Sep 18, 2025 06:42Balozi wa Marekani katika utawala wa kizayuni wa Israel, Mike Huckabee amesema, 'pamoja na Washington kuwa na washirika na marafiki kadhaa katika eneo la Mashariki ya Kati, "Israel ndiye mshirika wetu pekee wa kweli."