-
Israel yafuta mpango wa kushambulia Beirut baada ya onyo kali la Iran
Jun 02, 2026 09:12Utawala wa Israel umeachana na mpango wake wa kufanya mashambulizi makali ya ya kijeshi dhidi ya mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Haya yameelezwa siku ya Jumatatu na Rais wa Marekani, Donald Trump, kufuatia onyo kali kutoka kwa Iran kwamba haitavumilia wimbi jipya la uvamizi dhidi ya Beirut, hatua ambayo ingekiuka makubaliano ya kusitisha vita kati ya Iran na Marekani.
-
Mwanasiasa wa Ujerumani: EU ni mshirika katika ugaidi wa kimfumo wa Israel
Jun 01, 2026 02:55Mwanasiasa wa Ujerumani na mbunge wa zamani wa bunge la nchi hiyo amekosoa sera za utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema: "Walowezi wa Kizayuni wanafanya ugaidi wa kimfumo dhidi ya Wapalestina, na serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya wanashiriki katika uhalifu huo kwa kunyamaza kimya."
-
Waziri wa Israeli Ben-Gvir amhimiza Netanyahu 'kusawazisha vitongoji vya Beirut na ardhi'
May 31, 2026 12:48Waziri anayejiita wa usalama wa Israel, Itamar Ben-Gvir, amemtaka Waziri Mkuu wa utawaka huo katili, Benjamin Netanyahu, kusawazisha na ardhi vitongoji vya mji mkuu wa Lebanon, Beirut huku utawala huo ukizidisha mashambulizi yake dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iran yalaani ukiukaji wa Marekani wa makubaliano ya amani, yahimiza UN kuingilia kati
May 29, 2026 03:18Iran imelaani vikali vitisho vya mara kwa mara vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamisha vita haramu vya hivi karibun, ikiuhimiza Umoja wa Mataifa kuingilia kati.
-
Washington Post: Israel imetengwa duniani kutokana na vita vya mara kwa mara vya Netanyahu
May 29, 2026 02:57Gazeti la Washington Post limeandika kuwa: Vita vya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza, Lebanon, Syria, Iran na Yemen vimeiweka Israel katika njia ya mmomonyoko wa kijeshi, kushindwa kimkakati na kutengwa kimataifa.
-
Viwango vya Undumakuwili wa Ulaya; Kwa Nini Jinai za Israel Zinanyamaziwa Kimya?
May 22, 2026 15:20Hatua ya utawala wa Kizayuni ya kukamata meli 50 zilizokuwa zimebeba wanaharakati 428 wa haki za binadamu na misaada ya kibinadamu kutoka nchi 44 kwa ajili ya Wapalestina wanaozingirwa na utawala huo huko Gaza katika bahari ya Mediterania imeibua wimbi la hasira na chuki dhidi ya Wazayuni.
-
Picha za satalaiti zaonyesha uharibifu mkubwa kwenye kambi za kijeshi za Israel kutokana na mashambulizi ya Iran
May 22, 2026 14:53Picha mpya za satalaiti zilizochambuliwa zimefichua uharibifu na hasara kubwa iliyotokea katika vituo vingi vya kijeshi vya Israel kufuatia mashambulizi na operesheni za kujihami za Iran na harakati ya Lebanon Hizbullah na hivyo kuzusha maswali kuhusu ukubwa wa uharibifu ambao Tel Aviv inauficha mbele ya umma.
-
Intelijensia ya Iran yasambaratisha kundi la magaidi wa kitakfiri wenye uhusiano na Israel
May 20, 2026 02:50Timu za upelelezi za Iran zimefanikiwa kusambaratisha seli nne za wanamgambo wa Kitakfri wenye mfungamano na utawala wa Israel katika mkoa wa Sistan na Baluchistan, kusini mashariki mwa Iran mkoa unaopakana na Pakistan.
-
ICC yatoa hati “za siri” za kukamatwa kwa maafisa watano wa Israel
May 18, 2026 04:25Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yenye makao yake The Hague imeripotiwa kutoa hati tano za “siri” za kukamatwa kwa maafisa wa utawala wa Israel, wakiwemo wanasiasa watatu na maafisa wawili wa kijeshi.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran awaonya maadui, mkijaribu mtashindwa tena
May 15, 2026 09:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi, amezionya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuanzisha tena hatua mpya za kijeshi dhidi ya Iran, akisema kuwa makabiliano ya awali yalishindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa, na kwamba jaribio lolote la baadaye litakuwa na matokeo yaleyale.