-
Corbyn: Kuendelea Uingereza kuipa Israel silaha kunaifanya mshirika katika mauaji ya kimbari Gaza
Apr 01, 2024 07:14Kiongozi wa zamani wa chama cha Labour nchini Uingereza amezikosoa nchi za Magharibi - hasa Marekani na Uingereza - zinazoendelea kuipatia Israel silaha za kuwaua Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na kusema kuwa nchi hizo zinakiuka sheria za kimataifa.
-
Ufaransa, Misri na Jordan zapinga shambulio la Rafah na kuunga mkono usitishaji vita Gaza
Mar 31, 2024 22:47Mkutano wa pande tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Jordan na Ufaransa ulifanyika Jumamosi Cairo, mji mkuu wa Misri, kuhusiana na matukio ya hivi karibuni katika vita vya Gaza na mashauriano ya kusitisha mapigano hayo.
-
Licha ya kuikosoa Israel hadharani, Biden ameidhinisha kwa siri silaha mpya za kuwaulia Wapalestina
Mar 30, 2024 22:48Rais Joe Biden wa Marekani hivi karibuni ameidhinisha kwa siri kupatiwa utawala wa Kizayuni wa Israel silaha mpya za kivita zenye gharama ya mabilioni ya dola zikiwemo aina za kisasa za mabomu na ndege za kivita.
-
HAMAS: Misimamo ya Israel imekwamisha mazungumzo ya Doha
Mar 29, 2024 08:29Mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema mazungumzo ya kusimamisha vita katika Ukanda wa Gaza yamegonga mwamba huko Doha, mji mkuu wa Qatar kutokana na misimamo isiyoeleweka ya utawala haramu wa Israel.
-
Watu 38 wauawa katika hujuma za anga za Israel Syria, Iran yalaani
Mar 29, 2024 08:28Kwa akali watu 38 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya mji wa Aleppo (Halab) huko kaskazini mwa Syria.
-
Wamorocco waungana na Wajordan kuzitaka serikali zao zivunje uhusiano na Israel
Mar 29, 2024 04:30Maelfu ya watu wameandamana katika nchi za Jordan na Morocco kuonyesha mshikamano na Wapalestina ambao wamekuwa wakikabiliwa na vita vya kinyama vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa takriban miezi sita sasa, sambamba na kutoa wito kwa serikali zao wa kuvunja uhusiano na utawala huo ghasibu.
-
ICJ: Israel lazima ihakikishe msaada wa dharura, chakula vinaingizwa Ghaza bila kuchelewa
Mar 29, 2024 04:11Mahakama ya Juu zaidi duniani ya Haki ICJ imeuamuru utawala wa Kizayuni wa Israel "kuhakikisha msaada wa haraka wa kibinadamu" unaingizwa huko Ghaza bila kuchelewa, ikisisitiza kuwa "njaa imeshaingia" katika eneo hilo.
-
Erdogan: Dunia iishinikize Israel itekeleze azimio la Baraza la Usalama la UN
Mar 28, 2024 23:08Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ameitaka jamii ya kimataifa iendelee kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel utekeleze azimio la kutaka kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza, lililopasishwa majuzi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
CAIR: UN ichunguze jeshi la Israel lilivyowaua Wapalestina bila sababu na kuzifukia maiti zao
Mar 28, 2024 06:39Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani [CAIR] limetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchunguza video inayoonyesha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwapiga risasi bila sababuu Wapalestina wawili wanaoonekana kuwa hawana silaha kisha kuzifukia maiti zao kwa buldoza.
-
Haniya: Azimio la Baraza la Usalama linaonesha Israel imetengwa duniani
Mar 27, 2024 04:10Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umetengwa vibaya na dunia kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa; siku moja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupasisha azimio la kutaka kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza.