Apr 26, 2024 11:07 UTC
  • Bunge la EU ladhihirisha tena unafiki wa Magharibi kwa kulaani shambulio la kujibu mapigo la Iran dhidi ya Israel

Bunge la Ulaya limedhihirisha tena sera za undumilakuwili za Magharibi kwa kupitisha azimio la kulaani shambulio la hivi karibuni la kujibu mapigo lililofanywa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuzitolea wito nchi wanachama za umoja huo ziiwekee Tehran vikwazo vingine vipya na vikali zaidi.

Azimio hilo lililoungwa mkono kwa wingi mkubwa wa kura za wabunge 357 wa bunge la ulaya waliopiga kura za 'ndiyo' mkabala na 20 tu waliopinga limetilia mkazo tena uungaji mkono kamili wa taasisi hiyo ya Umoja wa Ulaya kwa ilichokiita usalama wa Israel na raia wake sambamba na kulaani hatua ya Tehran.

Wakati azimio hilo limedai kuwa Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) "wamechukizwa na shambulio" kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria na kusisitizia "umuhimu wa kuchungwa misingi ya kutokiuka kinga za majengo ya kidiplomasia na kibalozi," halikutaka ichukuliwe hatua yoyote kujibu jinai hiyo iliyofanywa na Israel, ambayo ilisababisha pia maafa ya roho za watu, lakini badala yake, limetaka viwekwe vikwazo zaidi dhidi ya Iran na washirika wake.

Operesheni ya "Ahadi ya Kweli" iliyotekelezwa na Iran kuutia adabu utawala wa Kizayuni

Azimio la Bunge la Ulaya limetaka pia Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC liwekwe kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi na kwamba uchukuaji wa hatua hiyo umechelewa sana ili kukabiliana na kile kilichodaiwa kuwa ni hatua haribifu za Iran.

Aidha limetoa wito wa kujumuishwa kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi mrengo wa kisiasa pia wa Harakati wa Hizbullah ya Lebanon kama ilivyofanywa kwa tawi la kijeshi la harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu.../ 

Tags