May 06, 2024 02:32 UTC
  • Borrell: Marekani imepoteza nafasi yake katika Nidhamu ya Dunia ya pande kadhaa

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema, Marekani imepoteza nafasi yake katika Nidhamu ya Dunia ya pande kadhaa.

Borrell ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa kwenye Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza na kubainisha kuwa Marekani haina tena mamlaka ya uamrishaji.
 
Mkuu huyo wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amefafanua kuwa katika miaka 30 iliyopita mchango wa China katika Pato Ghafi la Ndani Duniani umeongezeka kutoka asilimia sita na kukaribia 20%, wakati mchango wa nchi za Uaya umepungua kutoka 21% hadi 14% na Marekani kutoka 20% hadi 15%.

Borrell amekiri kwamba, China sasa inabadilika kuwa mshindani wa Ulaya na Marekani sio tu katika uzalishaji wa bidhaa za bei nafuu, lakini pia kwa kugeuka kuwa nguvu kubwa ya kijeshi iliyoko mstari wa mbele wa maendeleo ya teknolojia na ubunifu wa teknolojia zitakazoainisha muelekeo wa mustakabali wetu.

 
Inafaa kuashiria hapa kuwa China, ambayo ni nchi yenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani, inayotarajiwa kuipita Marekani na kuwa dola lenye nguvu kubwa zaidi za kiuchumi katika siku za usoni, ina mchango mkubwa katika juhudi na harakati za kuiondoa sarafu ya dola ya Marekani katika uga wa uchumi wa dunia.../

 

Tags