May 18, 2024 12:38 UTC
  • FAO: Hatua za kupunguza athari za El Nino kwa usalama wa chakula zimezaa matunda

Hatua zilizochukuliwa miaka miwili iliyopita na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ili kupunguza athari mbaya za mvua za El Niño katika nchi 23 duniani zimelinda usalama wa chakula na maisha ya watu zaidi ya milioni 1.6.

Hayo ni kwa mujiibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Mvua kubwa za El Nino zilizosababisha mafuriko makubwa na kutabiriwa kuendelea hadi katikati ya mwaka huu wa 2024 zimewaathiri watu milioni 50 duniani kote aghalabu yao wakiwa wa huko Amerika ya Latini na Caribbean, Asia na Pasifiki na katika maeneo ya kusini na mashariki mwa bara la Afrika. 

Mafuriko mashariki mwa Afrika 

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeeleza kuwa, lilichukua hatua za haraka kwa kushirikiana na serikali na mashirika mbalimbali katika nchi husika ili kupunguza athari mbaya za El Nino. 

Moja ya hatua zilizochukuliwa na shirika la FAo ni usambazaji mbegu zinazostahimili ukame kwa wakati na ujenzi wa vivuna maji katika maeneo makavu huko Amerika ya Latini, kufanyia marekebisho kingo za mito zilizovunjika huko Somalia ili kulinda hekta elfu 40 za mashamba dhidi ya mafuriko na kutumia programu za ulinzi jamii ili kuwasaidia wakulima walio katika mazingira magumu kwa kuwapatia misaada ya fedha. 

Maelfu ya watu katika nchi za Afrika Mashariki wamelazimika kuhama maeneo waliyokuwa wamepata hifadhi kufuatia  mvua kubwa ambazo zimesababisha mafuriko yaliyoambatana na maafa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNCHR) limetaja wakimbizi walioathiriwa kuwa ni wale walioko Tanzania, Kenya, Somalia na Burundi. 

Tags