Jul 02, 2024 07:54 UTC
  • Jeshi la Israel lasema liko tayari kusimamisha vita dhidi ya Gaza mwezi huu

Maafisa wa kisiasa wa utawala ghasibu wa Israel wamesema jeshi la utawala huo liko tayari kutekeleza hatua kwa hatua hatua ya tatu na hatimaye kuhitimisha vita dhidi ya Ukanda wa Gaza mwezi huu wa Julai.

Shirika la Redio na Televisheni ya utawala wa Kizayuni limesema kuwa, hatua ya tatu ya vita dhidi ya Ukanda wa Gaza inajumuisha kubakia wanajeshi wa Kizayuni katika eneo la Philadelphia, mipaka ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) na Misri katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kivuko cha "Netsarim," maeneo ambayo yanatumiwa na wavamizi kutenganisha maeneo ya kaskazini na ya kusini mwa Gaza, ili eti kutoa mashinikizo dhidi ya wanaharakati wa Muqawama wa Kiislamu wa Palestina, Hamas.

Kwa mujibu wa ripoti hii, uamuzi wa kumaliza vita dhidi ya Gaza umechukuliwa eti kutokanma na makubaliano ya kubadilishana mateka na ghasia na mapigano yanayoendelea kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu, ili kuzuia kuenea vita katika maeneo mengine ya Palestina.

Kabla ya hapo gazeti la "Wall Street Journal" katika ripoti iliyowanukuu wachambuzi wa masuala ya usalama, liliandika kuwa shambulio la jeshi la utawala wa Kizayuni katika kitongoji cha "Al-Shaja'iyya", kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, limethibitisha wazi kuwa "kufutwa" Harakati wa Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, hakuwezekani kirahisi.
 

Maafa na madhara makubwa ya vita vya Gaza kwa jeshi la Israel

Baada ya kupita takriban miezi 9 tangu utawala wa Kizayuni uvamie Ukanda wa Ghaza bila ya mafanikio yoyote, utawala huo unazidi kuzama katika migogoro ya ndani na nje siku baada ya siku.

Katika kipindi hiki, utawala huo wa kigaidi haujapata mafanikio yoyote isipokuwa kuendelea kutekeleza jinai za kivita, mauaji ya umati, uharibifu, ukiukaji wa sheria za kimataifa, ulipuaji wa mashirika ya misaada ya kibinadamu na kusababisha njaa katika ukanda huo unaozingirwa na Wazayuni.

Bila kujali mafanikio ya baadaye, utawala wa Israel tayari umeshindwa katika vita hivyo, ambapo hata baada ya kupita takriban miezi 9 ya mashambulizi ya kinyama dhidi ya raia wa kawaida wasio na hatia, haujaweza kuyafanya makundi ya muqawama wa Palestina, yasalimu amri katika eneo dogo ambalo limezingirwa kwa miaka mingi, na tayari umepoteza uungaji mkono wa kimataifa kutokana na jinai za kivita na mauji ya umati unaotekeleza huko Gaza.

Tags