Jun 13, 2024 12:07 UTC
  • Iran: Mataifa ya Kiislamu yanapaswa kutumia suhula zote ili kusitisha jinai za Wazayuni Gaza

Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran haitawaruhusu wavamizi wa Kizayuni kudhoofisha uthabiti na usalama wa eneo hata kwa chembe moja.

Ali Bagheri Kani amesema hayo leo mjini Baghdad katika mkutano wake wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake Fuad Hussein, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq na kusisitiza kwamba, mataifa ya Kiislamu yanapaswa kutumia kila suhula yalizonazo ili kusitisha jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Bagheri Kani amesema kwamba, leo tunashuhudia mauaji ya halaiki huko Gaza, lakini watu wanaodhulumiwa wa Gaza wananyanyua bendera ya ushindi kutoka chini ya vifusi hivyo sisi tunasisitizia udharura wa kutumiwa uwezo wa mataifa ya Kislamu ili kukomesha uhalifu dhidi ya watu wa Gaza wasio na hatia.

Mkutano na waandishi wa habari wa Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran (kushoto) na Fuad Hussein, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq

 

Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekosoa undumakuwili wa Marekani na kueleza kwamba, Marekani haiwezi kuwapa Wazayuni silaha za hali ya juu kwa upande mmoja, na wakati huo huo etii inataka kushikamana na mpango wa kisiasa wa utatuzi wa mgogoro huo.

Kwa upande wajke, Fuad Hussein, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq amesema kuhusu hali ya Gaza: Hatuhitaji usitishaji vita kwa muda, bali tunahitaji usitishaji vita wa kudumu huko Gaza. Kadhalika amesema, "tunaunga mkono kufikiwa kwa usitishaji vita wa kudumu huko Gaza. Hali ya usalama katika eneo hili inazidi kuzorota na tunaonya dhidi ya kuenea kwa vita."

Tags