Mar 06, 2024 07:34 UTC
  • Afisa wa FAO: Ulaya yakabiliwa na upungufu wa chakula huku bei zikiongezeka kimataifa

Afisa wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ametanagza kuwa matukio yanayojiri katika Bahari Nyekundu na katika mlango bahari wa Bab Al-Mandab yameathiri biashara ya chakula duniani na kusababisha ongezeko la bei kimataifa.

Oleg Kobyakov Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Russia katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ameongeza kuwa, matukio yanayojiri katika Bahari Nyekundu na mlango wa bahari wa Bab al-Mandab kwa upande mmoja, na migomo mikubwa ya  wakulima barani Ulaya kwa upande mwingine, yameathiri biashara ya chakula duniani na kusababisha ongezeko la bei kimataifa. 

Kobyakov amesema kuwa: kufungwa  mlango  bahari wa Bab al-Mandab na matukio yanayoendelea katika Bahari Nyekundu yamekuwa na athari mbaya kwa biashara ya chakula duniani, huku safari za meli katika njia hiyo ya majini zikipungua kwa asilimia 30, lakini gharama ya kukodisha meli imeongezeka mara nne.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Russia katika shirika la FAO ameashiria pia mgomo mkubwa wa wakulima barani Ulaya na uwezekeno wa kufutwa na kupunguzwa ruzuku ya mafuta na misaada mingine ya serikali kwa sekta ya kilimo na kutahadharisha kuhusu upungufu wa chakula katika bara hilo.  

Tags