Jul 01, 2024 08:17 UTC
  • Wall Street Journal: Makosa ya Marekani yameifanya Iran kuwa nchi muhimu kimataifa

Jarida la Wall Street Journal la nchini Marekani limeandika katika ripoti yake mpya kwamba: Licha ya mashinikizo ya miongo kadhaa kutoka kwa nchi za Magharibi, lakini Tehran inaendelea kuwa tishio kwa maslahi ya Marekani kutokana na uhusiano wake mzuri na Russia na China.

Katika ripoti yake hiyo mpya, jarida la Wall Street Journal limeeleza kuwa, Iran ina ushawishi unaoongezeka katika anga za kimataifa, kuliko miongo kadhaa iliyopita.

Jarida hilo maarufu la Marekani pia limeandika: Iran, chini ya uongozi wa Ayatullah Khamenei, imepambana na mashinikizo ya Marekani kwa miongo kadhaa na Marekani na madola ya Magharibi yameshindwa kuifanya Iran itengwe bali Tehran imeongeza kiwango cha kupambana na Washington.

Makala hiyo ya jarida la Wall Street Journal imedai kuwa, ingawa vikwazo vimeusababishia matatizo uchumi wa Iran, lakini mikataba baina ya Tehran na China na Russia imeleta manufaa ya kifedha na kidiplomasia kwa Jamhuri ya Kiislamu. Iran pia imetumia vizuri fursa ya miongo kadhaa ya makosa ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi kuimarisha ushawishi wake. 

Jarida hilo la Marekani aidha limeandika kuwa, Iran leo hii ni imara zaidi kuliko wakati mwingine wowote tangu yalipofanyika Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979 na ni tishio kubwa kwa maslahi ya Marekani na washirika wake katika ukanda wa Asia Magharibi.

Pia limeandika: "Nguvu za kijeshi za Iran ni pana, ni za kina zaidi na ni kubwa kuliko huko nyuma.