Jul 03, 2024 03:47 UTC
  • Ripoti: Kiwango cha wawekezaji wa nje barani Afrika kimeshuka

Imeelezwa kuwa, Afrika haikuvutia sana uwekezaji wa kigeni mwaka jana (2023) na makubaliano ya kifedha yalishuka kwa asilimia 50 mpaka dola bilioni 64, kwa mujibu wa ripoti mpya.

Ripoti ya World Investment iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo inaonyesha kuwa, uwekezaji wa kigeni unatokana na kupungua kwa kasi ya uchumi ulimwenguni na kuongezeka kwa mivutano ya kisiasa kijiografia.

Katika bara hilo, nchi za Afrika ya Kati zimerekodi kushuka kwa idadi kubwa sana, asilimia 17, na Afrika Magharibi imerekodi kiwango cha chini sana mpaka asilimia moja.

Bruce Nsereko-Lule ni mshirika mkuu katika Seedstars Africa Ventures, kampuni ya ubia ya mitaji ambayo inawekeza katika makampuni yenye ukuaji wa juu.

Anasema hali ya uchumi katika mataifa ya Magharibi imechangia kupunguza kwa uwekezaji kutoka nje ya bara hilo. Aidha amesema, uwekezaji katika masoko haya ya maendeleo, masoko yanayoibukia yamekuwa hayavutii sana wakati makampuni yanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuwa na uzalishaji mzuri ambao utafanya kuwepo na hali nzuri kwa wawekezaji wa Magharibi.

Kupungua kwa uwekezaji wa kigeni kunalaumiwa kwa sera za ulinzi za serikali za Kiafrika na marekebisho ya kikanda, ambayo wachunguzi wanasema yanavuruga uchumi wa dunia, yanavunja mitandao ya biashara, na mifumo ya udhibiti wa mazingira na usambazaji wa kiamtaifa.

Baadhi ya hatua za serikali zimedhoofisha uthabiti na kutabiri kwa mtiririko wa uwekezaji wa kimataifa, na kuleta vikwazo na kutenga fursa.