Jul 01, 2024 08:07 UTC
  • Wanaharakati wa Iraq waipiga tena kwa makombora bandari ya Eilat ya utawala wa Kizayuni

Wanaharakati wa Muqawama wa Iraq wamesema kuwa wamefanya shambulizi jipya dhidi ya Bandari ya Eilat katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu Wazayuni na ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.

Wanaharakati wa Muqawama wa Iraq wameshambulia Bandari ya Eilat kwa kutumia ndege zisizo na rubani, imesema taarifa hiyo.

Wanaharakati wa Muqawama wa Iraq wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya Israel tangu utawala huo unaoukalia kwa mabavu ardhi ya Palestina ulipoanzisha vita vya mauaji ya halaiki huko Ukanda wa Gaza mapema mwezi Oktoba 7, mwaka jana 2023.

Wanaharakati  wa Muqawama wa Iraq wafanya mashambulizi   katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel

Wanaharakati  wa Muqawama wa Iraq  pia wamekuwa wakipiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq na katika nchi jirani ya Syria ikiwa ni kulipiza kisasi uungaji mkono wa Washington kwa mauaji ya kimbari ya Israel wa Gaza.

Utawala katili wa Israel umekuwa ukifanya mashambulizi makali dhidi ya Ukanda wa Gaza, yakilenga hospitali, makazi ya raia na nyumba za ibada baada ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) kuendesha operesheni ya kishujaa ya Kimbunga cha Al-Aqsa Oktoba 7, 2023, mwaka jana na kutoa pigo kubwa kwa utawala wa Kizayuni ambao ulikuwa unajigamba kuwa haupigiki na haushindiki.

Tags