Jul 01, 2024 02:22 UTC
  • Gazeti la Kizayuni la Haaretz: Vita na Hizbullah ni

Gazeti moja la Kizayuni linalochapishwa mjini Tel Aviv limetabiri kuwa, matokeo ya vita vikubwa kati ya utawala wa Kizayuni na Hizbullah ya Lebanon ni sawa na kujitia kitanzi Israel na kushindwa vibaya sana.

Hali ya wasiwasi imezidi kuwa kubwa katika mpaka wa Lebanon na ardhi za kaskazini mwa Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel na mara kwa mara serikali ya Netanyahu imekuwa "ikijipiga kifua" kwamba itaingia kwenye vita vikubwa na Hizbullah ya Lebanon lakini muda wote duru zenyewe za Kizayuni zimekuwa zikimuonya vikali Netanyahu na kundi lake kwamba kuingia vitani na Hizbullah ni kuiangamiza Israel. 

Kwa mujibu wa IRNA, gazeti la "Haaretz" la Israel limeonya katika ripoti yake ya karibuni kabisa yenye kichwa cha maneno "Matokeo ya vita na Lebanon ni kushindwa vibaya mno" kwamba Israel itapata pigo kubwa sana iwapo vita vitapanuka hadi Lebanon.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz

 

Vile vile gazeti hilo la Israel limeandika kuwa, pamoja na kwamba baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu halikuwa na nia ya kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya Lebanon katika kipindi cha miezi minane iliyopita, lakini wapinzani wa kisiasa wa Netanyahu wamefichua kuhusu masaibu ya wakaazi wa kaskazini mwa ardhi za Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Mashambulizi ya makombora na droni (ndege zisizo na rubani) ya Hezbollah katika eneo hilo yamefanya hali yake kuwa ngumu mno.

Kwa mujibu wa gazeti hilo la Israel, utawala ghasibu wa Kizayuni hauna uwezo hivi sasa wa kufanya mashambulizi makubwa dhidi ya Lebanon wala kuteka maeneo ya kusini mwa nchi hiyo, bali unataka tu kufanya operesheni ndogo ya kijeshi kwenye mpaka, lakini jibu la Hizbullah kwa hatua yoyote ya kijeshi ya Israel linaweza kuwa kubwa mno na angamizi.

Tags