May 06, 2024 10:44 UTC
  •  Abdelmadjid Tebboune
    Abdelmadjid Tebboune

Rais wa Algeria amesema, ubinadamu umepoteza nyanja zote za kiutu na ustaarabu katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Rais Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, ameyasema hayo katika mkutano wa 15 wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu mjini Banjul, mji mkuu wa Gambia, na ameiomba jamii ya kimataifa na watu wote huru na wenye dhamiri hai duniani kuchukua hatua za kukomesha maafa yanayowapata watu wa Palestina hususan katika Ukanda wa Gaza.

Abdelmadjid Tebboune amesema yanayofanywa na Wazayuni dhidi ya wananchi wa Palestina hususan katika Ukanda wa Gaza ni vita vya mauaji ya kimbari na kuongeza kuwa, mashirika na taasisi za kimataifa zimeshindwa kutekeleza maazimio ya kimataifa, hasa Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu mkabala wa jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni.Gaza

Israel inaendelea kuua watoto wa Gaza

Katika kikao chake cha mwisho huko banjuul jana Jumapili, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ilitoa wito wa kufanyika uchunguzi huru kuhusu jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Israel huko Gaza. OIC Imetaja jinai hizo kuwa ni "uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu".

Kadhalika viongozi wa OIC waliohudhuria mkutano humo nchini Gambia wametaka kuwajibishwa na kubebeshwa dhima utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

Tags