Apr 27, 2024 11:44 UTC
  • Wachambuzi: Maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu Marekani yanamuweka Biden matatani

Duara la maandamano ya wanafunzi wa vyuo viku dhidi ya vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza linazidi kupanuka nchini Marekani, na kusababisha mkanganyiko mkubwa katika hesabu za Israel na waungaji mkono wake.

Maandamano na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani pia yamesababisha mkanganyiko mkubwa katika mahesabu ya utawala wa Joe Biden, ambao waandamanaji wanasema unahusika na jinai zinazofanywa dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Mtafiti katika Taasisi ya Mashariki ya Kati, Dk. Hassan Mneimneh anasema: "Kinachotokea katika vyuo vikuu vya Marekani ni tishio kubwa kwa simulizi inayoiunga mkono Israel huko Marekani, kwa sababu wanafunzi hao wanatetea maadili ya kusimama pamoja haki na wanaokandamizwa, na kuwatetea Wapalestina na haki zao.

Dk. Hassan Mneimneh anasema, kinyume chake, mamlaka rasmi, kwa sababu ya kuogopa harakati za wanafunzi, inawataja waandamanaji kuwa ni waovu na mashetani, na kutambua ukosoaji wa aina yoyote dhidi ya Israel kuwa marufuku katika majimbo mengi ya Marekani.

Kwa muktadha huo, Dk. Mneimneh anaashiria kuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Mike Johnson, amepinga kupandisha bendera za Palestina katika vyuo vikuu na kukariri uongo unaoenezwa na utawala ghasibu wa Israel.

Vilevile viongozi wa Marekani wanataka kuzima maandamano hayo ya kuwatetea Wapalestina kwa kudai kuwa wanafunzi wanaoandamana wana chuki dhidi ya Wayahudi na kwamba wanaunga mkono ugaidi!

Charles Dunn, mjumbe wa zamani wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani, anaunga mkono haki ya wanafunzi kueleza misimamo yao, kupinga mauaji yanayofanyika Gaza na kutetea haki za watu wa Palestina, akisema kuwa harakati zao za maandamano zina athari kwa mwamko wa kisiasa nchini Marekani.

Image Caption

Ni vyema kuashiria hapa kuwa, kampeni ya maandamano katika vyuo vikuu vya Marekani mwaka 1968 dhidi ya Vita vya Vietnam ilikuwa na athari kubwa katika uchaguzi wa rais wakati huo. Kwa misngi huo, Charles Dunn anaona kwamba, hali hii inaweza kujikarir iwapo maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani kuhusu Gaza yataendelea.

Tags