May 07, 2024 11:38 UTC
  • Meja Jenerali Salami: Ikiwa Waislamu wataacha jihadi basi wataishi kidhalili

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (SEPAH) amesema kuwa, ubeberu unaamiliana na ulimwengu wa Kiislamu kwa sera na siasa moja na wala haujali mipaka na kusisitiza kuwa, iwapo adui atadhibiti eneo la Kiislamu basi atapanua hadi sehemu nyingine.

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa SEPAH amesema hayo mjini Damscus Syriia katikak shughuli ya Arobaini ya mashahidi wa ubalozi mdogo  wa Iran mjini humo na kusisitiza kwamba, uistikbari unatakka kudhibiti utambulisho wa Kiislamu.

Meja Jenerali Salami ameongeza kuwa, sisi Waislamu tuko katika meli moja na tuna mahusiano na mafungano sisi kwa sisi na endapo Waislamu wataacha jihadi, basi wataishi kwa udhalili.

Kadhalika Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (SEPAH) ameeleza kuwa, njia na hatima yetu ni moja na hatuwezi kuishi kwa kugawanyika, kwa sababu ikiwa adui atadhibiti eneo la Kiislamu, atapanua udhibiti huo hadi eneo jingine, na kwa hiyo ni lazima tulinde na kuhifadhi vipengele na vielelezo vya nguvu tunayomiliki.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (SEPAH)

 

Tarehe Mosi Aprili 2024, utawala wa Kizayuni wa Israel ulifanya jinai ya kushambulia ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria ambao kwa mujibu wa sheria zote za kimataifa, hiyo ni sehemu ya ardhi ya Iran.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilifuatilia suala hilo katika jamii ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa lakini nchi tatu za Magharibi yaani Marekani, Uingereza na Ufaransa zililizuia Baraza la Usalama kulaani jinai hiyo ya Israel.

Ni kwa sababu hiyo ndio maana Jumamosi usiku, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilifanya shambulizi kubwa dhidi ya Israel na kupiga na kusambaratisha kambi ya kijeshi iliyotumika kushambulia ubalozi wake wa Damascus ikiwa ni haki ya kisheria ya Iran kujibu jinai hiyo.