May 07, 2024 11:35 UTC
  • Wapalestina 20 wauawa shahidi katika muendelezo wa unyama wa Wazayuni huko Gaza

Wapalestina 20 wameuawa shahidi kutokana na mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.

Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA) linaripoti kuwa, katika siku ya 214 ya vita vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, mizinga, helikopta na vifaru vya utawala wa Kizayuni vimefanya mashambulio katika maeneo ya mashariki ya Rafah.

Taarifa iliyotolewa na Izzuddin Qassam Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema wapiganaji wake wamewashambulia wanajeshi wa Israel kwa makombora mapema siku ya Jumanne kwenye mpaka wa Kerem Shalom, ambao ulikuwa umefungwa kutokana na mashambulizi ya maroketi ya mwishoni mwa wiki.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Ismail Haniyah Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema amewasilisha jibu la Hamas kwa mpango uliopendekezwa wa pamoja wa Misri na Qatar kuhusu kukomesha mashambulizi ya utawala wa Israel, kubadilishana mateka na kuondoa vikwazo na mzingiro dhidi ya Gaza.

Image Caption
Jeshi katili la Israel limeua takriban Wapalestina 35,000 huko Gaza tangu lianzishe mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo  Oktoba 7, 2023

 

Taarifa fupi kutoka kwa Hamas siku ya Jumatatu ilisema kuwa harakati hiyo imekubali pendekezo la kusitisha mapigano huko Gaza, ambako imekuwa ikikabiliana na utawala vamizi wa Israel kwa miezi saba.

Jeshi katili la Israel limeua takriban Wapalestina 35,000 huko Gaza tangu lianzishe mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo  Oktoba 7 mwaka jana. Idadi kubwa ya waliouawa ni wanawake na watoto.

Tags