May 09, 2024 02:33 UTC
  • Raisi: Iran kamwe haitaruhusu kutengwa wanawake katika jamii

Rais wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu katu haitakubali sera ambazo zitapelekea kutengwa wanawake katika jamii.

Rais Ebrahim Raisi alisema hayo jana Jumatano akihutubia mkusayiko wa mabanati wadogo wa Kiirani hapa Tehran, siku mbili kabla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mazazi ya Hadhrat Maasuma SA, ambayo hutambuliwa kama Siku ya Mtoto wa Kike hapa nchini.

Rais Raisi ameeleza bayana kuwa, Iran haitakubali kuburuzwa na kufuata mienendo na utamaduni wa nchi za Magharibi wa kumtazama mwanamke kama chombo. 

Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatilia maanani umuhimu wa kuweka mazingira salama kwa wanawake kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii.

Aidha Sayyid Raisi amepongeza maendeleo yaliyofikiwa na wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hatua zinazochukuliwa na serikali ya Tehran ili kuwawezesha wanawake hapa nchini.

"Tunapinga mtazamo wa kumuweka mbali mwanamke na jamii na kumzuia kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii," amesisitiza Rais Ebrahim Raisi wa Iran.

Tags