May 08, 2024 12:00 UTC
  • Msemaji wa Guterres: Hakuna mtu aliye na haki ya kuitishia Mahakama ya kimataifa ya Jinai (ICC)

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa missada inapasa kuingia Ukanda wa Gaza bila ya kizuizi chochote na kwamba upande wowote haupasi kutoa vitsho kwa wafanyakazi wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

Stephen Dujarric Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko New York kuwa wafanyakazi wa umoja huo waliopo Gaza wanendelea kutoa huduma katika maeneo yenye vita na bado wapo huko. Ameongeza kuwa, hakuna upande wowote ulio na haki ya kuwatishia wafanyakazi wa Mahakama ya Kimataifa ya  Jinai ICC. 

Maseneta 12 wa chama cha Republican nchini Marekani wameitishia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwamba wataiadhibu vikali najakama hiyo endapo itatoa waranti wa kumtia nguvuni Benjamini Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza. 

Mseneta wa Marekani walioitishia ICC 

Waungaji mkono wa Israel katika vyama viwili vya Democrat na Republican ndani ya Kongresi ya Marekani pia wametahadharisha kuwa endapo mahakama ya ICC itatoa hukumu dhidi ya Netanyahu na utawala wa Kizayuni basi taasisi hiyo ya sheria itakabiliwa na hatua za Marekani. 

Utawala wa Kizayuni wa Israel huku ukiungwa mkono na kupata himaya ya pande zote ya Marekani huku mashirika ya kimataifa yanayodai kutetea haki za binadamu yakiwa yamekaa kimya, kwa miezi saba sasa unaendelea kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza.