May 08, 2024 03:16 UTC
  • Nasser Kan'ani
    Nasser Kan'ani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali mashambulizi ya utawala unaotekeleza mauaji ya kimbari wa Israel katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Nasser Kan'ani amelaani vikali mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika mji wa Rafah na kueleza kuwa, utawala ghasibu unatekeleza mashambulizi hayo kwa lengo la kukwamisha juhudi za kimataifa za kusimamisha vita na kuhitimisha mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala huo katika Ukanda wa Gaza, na kwa nia ya kulinda maslahi ya mtu binafsi na ya kundi la wahalifu wa utawala ghasibu wa Kizayuni. 

Kan'ani amesisitiza kuwa, ufunguo wa amani na usalama katika eneo la Magharibi mwa Asia ni kusitishwa mara moja na bila ya masharti vita vya utawala bandia wa Israel dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan; na pande zote husika kimataifa zinapasa kuuwekea mashinikizo utawala ghasibu wa Israel kwa ajili ya lengo hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, bila shaka utawala wa Kizayuni unaouwa watoto na muungaji mkono wake mkuu yaani serikali ya Marekani, ndio wanaopasa kubeba dhima na kuwajibika mbele ya jinai na umwagaji damu unaoendelea sasa katika mji wa Rafah; na watendaji jinai hawa wanapsa kutoa majibu mkabala wa jinai hizo. 

Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kushambulia maeneo ya mashariki mwa mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza tangu jana Jumanne. 

Mashambulizi ya umwagaji damu ya Israel katika mji wa Rafah 

Hadi sasa makumi ya watu wameuawa shahidi na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo ya umwagaji damu.