-
Lebanon kuishtaki Israel katika Baraza la Usalama kwa kuishambulia kwa droni
Feb 15, 2024 23:16Serikali ya Lebanon imesema itawasilisha faili la malalamiko dhidi ya Israel katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kufuatia hatua ya utawala huo wa Kizayuni kufanya shambulio hatarishi la ndege zisizo na rubani na kuua watu kadhaa kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Hizbullah yaapa kujibu mashambulizi ya Israel yaliyoua raia wakiwemo watoto wawili
Feb 15, 2024 04:19Afisa wa ngazi ya juu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amelaani mashambulizi ya hivi karibuni zaidi ya Israel kusini mwa Lebanon yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa wakiwemo watoto wawili, ikiapa kwamba majibu ya harakati ya Muqawama ya Lebanon yako njiani.
-
Ombi la Afrika Kusini kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu jinai za Israel katika mji wa Rafah, Gaza
Feb 14, 2024 10:28Serikali ya Afrika Kusini imesema imeiomba Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuzingatia iwapo uamuzi wa utawala wa Israel kupanua operesheni za kijeshi Gaza hadi mji wa huko Rafah utahitaji mahakama hiyo kutumia mamlaka yake kuzuia ukiukwaji zaidi wa haki za Wapalestina.
-
Netanyahu apinga pendekezo la kufikia makubaliano na HAMAS
Feb 14, 2024 04:04Waziri Mkuu wa Israel amepuuzilia mbali pendekezo la mashirika ya kijasusi ya Mossad na Shin Bet ya utawala huo wa Kizayuni juu ya kufikia mapatano ya kubadilishana wafungwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
-
Kuongezeka ukosoaji wa Magharibi dhidi ya himaya ya Marekani kwa Israel katika vita vya Gaza
Feb 13, 2024 23:06Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, Jumatatu iliyopita aliitaka Marekani kuacha kutoa silaha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na kiwango kikubwa cha mauaji ya raia katika vita vya Gaza.
-
Ripoti ya Amnesty: Inayamkinika Israel imefanya uhalifu wa kivita Rafah
Feb 13, 2024 04:06Amnesty International ya Uingereza imefichua ushahidi wa "mashambulizi yasiyokubalika kisheria" ya mauaji yaliyofanywa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel katika mji wa Rafah, Gaza, na kueleza kwamba jeshi la utawala huo limetenda uhalifu wa kivita na ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu wakati wa mashambulizi ya kikatili katika eneo hilo.
-
Mkuu wa Sera za Nje wa EU ataka upelekaji silaha kwa Israel ukomeshwe ili kupunguza maafa Gaza
Feb 13, 2024 03:52Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametoa wito kwa washirika wa utawala wa Kizayuni Israel kukomesha upelekaji silaha kwa utawala huo ghasibu iwapo wanataka kupunguza vifo vya raia vinavyosababishwa na vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Vita vya maneno kati ya Misri na Israel vinaendelea baada ya Tel Aviv kuihusisha Cairo na Oktoba 7
Feb 13, 2024 02:58Mvutano wa kidiplomasia kati ya Misri na utawala wa Kizayuni wa Israel umeongezeka kufuatia matamshi yenye utata yaliyotolewa na waziri wa Israel ya kuihusisha Cairo na matukio ya Oktoba 7.
-
Mahakama ya Uholanzi yaiamuru Serikali isimamishe kuipatia Israel vifaa vya ndege za kivita
Feb 12, 2024 08:01Mahakama ya Uholanzi imeiamuru serikali kusitisha utoaji wa vifaa na vipuri vya ndege za kivita za F-35 zinazotumiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashambulizi yake ya kinyama unayofanya katika Ukanda wa Gaza.
-
Maandamano makubwa yafanyika Rabat kupinga uhusiano wa Morocco na Israel 'mfanya mauaji ya kimbari'
Feb 12, 2024 07:30Maelfu ya Wamorocco wamejitokeza tena kwenye barabara za mji mkuu wao Rabat kutoa wito wa kusitishwa uhusiano wa nchi yao na utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao wameulaani na kuutaja kuwa kuwa ni mfanya "mauaji ya kimbari" katika Ukanda wa Gaza.