Pars Today
Wizara ya Ulinzi ya Italia imekadhibisha madai ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rome ina mpango wa kuongeza idadi ya wanajeshi wake nchini Libya.
Watu wa Italia wameshiriki katika maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Roma kwa lengo la kutangaza uungaji mkono wao kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina sambamba na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Leo ni Jumatano tarehe 21 Mfunguo Mosi Shawwal 1442 Hijria inayosadifiana na tarehe Pili Juni mwaka 2021.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Ufaransa, Ujerumani na Italia Alkhamisi iliyopita walikwenda Tripoli mji mkuu wa Libya kwa shabaha ya kujadili mustakbali wa uhusiano wa nchi za Ulaya na Libya. Mawaziri hao pia wamesisitiza udharura wa kuondoka vikosi vya majeshi ya kigeni katika ardhi ya Libya.
Serikali ya Italia imesema kuwa inaunga mkono kikamilifu juhudi za kurejesha amani na utulivu katika nchi ya kaskazini mwa Afrika ya Libya.
Serikali ya Italia imesimamisha uuzaji wa silaha kwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, baada ya wanaharakati na wabunge wa nchi hiyo ya Ulaya kuonya kuwa, silaha hizo zinatumika kukanyaga haki za binadamu nchini Yemen.
Leo ni ijumaa tarehe 20 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1442 Hijria inayosadifiana na tarehe 6 Novemba mwaka 2020.
Muungano wa mashirika na jumuiya za kiuchumi za Italia umezungumzia athari mbaya za janga la corona yaani COVID-19 katika uchumi wa nchi hiyo na kusema kuwa, uchumi wa Italia umeporomoka vibaya na umerejea katika hali uliyokuwa nayo miaka 20 iliyopita.
Leo ni Jumamosi tarehe 29 ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani 1441Hijria sawa na tarehe 23 Mei 2020 Miladia.
Taasisi ya Usalama wa Kijamii nchini Italia imesema kuwa, idadi kamili ya watu waliopoteza maisha kutokana na virusi vya Corona kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu ni zaidi ya watu elfu 19 waliotangazwa rasmi na serikali.