-
Watu 12 wauawa katika hujuma za wanamgambo wa ADF nchini DRC
Jan 26, 2022 08:37Watu wasiopungua 12 wameuawa katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia mashambulio ya waasi wa Uganda wa ADF.
-
Wakazi wa Beni DRC waandamana wakitaka kuondolewa mzingiro
Jan 25, 2022 04:23Mtu mmoja ameuawa huku wengine 30 wakikamatwa na maafisa usalama katika maandamano ya wakazi wa mji wa Beni wanaoshinikiza kuondolewa 'hali ya mzingiro' katika majimbo ya kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaliyokumbwa na machafuko na mauaji ya mara kwa mara ya magenge ya waasi.
-
DRC yawakamata wanaotuhumiwa kumuua balozi wa Italia
Jan 20, 2022 00:54Vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimewatia nguvuni watu wawili wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa balozi wa Italia nchini humo.
-
Maandamano kwa ajili ya kuachiliwa huru mfungwa wa kisiasa wa serikali ya Congo DRC
Jan 19, 2022 08:25Maandamano yalifanyika jana Jumanne huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya kushinikiza kuachiliwa huru mfungwa mashuhuri wa kisiasa wa serikali ya Kinshasa ambapo makumi ya watu walikeruhiwa katika maandamano hayo.
-
Naibu Spika wa Bunge la DRC ajiuzulu kwa 'kudhalilishwa'
Jan 15, 2022 08:19Naibu Rais wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kile alichokitaja kuwa udhalilishaji na ukandamizaji.
-
Wanyarwanda wapatao 100 wakimbilia Kongo DR kukwepa chanjo ya Covid-19
Jan 13, 2022 00:42Raia wa Rwanda wapatao 100 wamevuka mpaka na kuingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa kile wanachosema, wanakimbia nchi yao kwa sababu ya kushurutishwa kupiga chanjo, ili kupambana na janga la Covid-19.
-
Wanajeshi wa Burundi 'waonekana' mashariki mwa Kongo DR
Jan 05, 2022 23:20Wanajeshi wa Burundi wameripotiwa kuingia katika ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
DRC yaangamiza ugonjwa wa meningitis Tshopo
Dec 25, 2021 05:12Hatimaye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imetangaza kuwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo au meningitis katika jimbo la Tshopo kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo, umetokomezwa.
-
UN yaiongezea MONUSCO muda wa kuhudumu nchini Kongo DR
Dec 21, 2021 23:13Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeuongezea muda wa mwaka mmoja Ujumbe wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO na kuwataka walinda amani wa ujumbe huo kuelekeza nguvu zao Kaskazini-Mashariki mwa nchi, huku likisisitizia kufanyika operesheni za pamoja na vikosi vya nchi hiyo, FARDC.
-
Wakazi wa Goma wapinga kupelekwa polisi wa Rwanda katika mji huo
Dec 20, 2021 23:11Mamia ya wakazi wa mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefanya maandamano kupinga kupelekwa askari polisi wa Rwanda katika mji huo.