-
Zarif aonesha hisia zake kufuatia miaka mitatu ya kujitoa Marekani katika JCPOA
May 09, 2021 01:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonesha hisia zake kufuatia miaka mitatu ya kujitoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba miaka mitatu iliyopita, kulizuka "kinyago cheusi" katika ahadi za Marekani ndani ya ndani ya azimio nambari 2231 na mapatano ya JCPOA baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano hayo.
-
Araqchi: Kumefikiwa mapatano ya kuondoa aghalabu ya vikwazo dhidi ya Iran
May 02, 2021 03:06Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kikao cha jana cha Tume ya Pamoja ya Mapatano ya Nyuklia ya JCPOA na kusema kikao hicho kimefikia mwafaka kuhusu kuondolewa Iran vikwazo.
-
Putin ataka kuhuishwa JCPOA katika muundo wake wa asili
May 01, 2021 08:46Rais Vladmir Putin wa Russia ametoa mwito wa kuhuishwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kuyarejesha katika muundo wake wa asili.
-
Mazungumzo ya Vienna, maendeleo na changamoto zake
Apr 28, 2021 05:35Katika fremu ya utekelezaji wa hatua za kistratijia kwa ajili ya kufuta vikwazo vya kidhalimu na kulinda maslahi ya taifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilichukua hatua za kulipiza kisasi ikijibu hatua ya Marekani na kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na vilevile hatua ya nchi za Ulaya ya kutotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa makubaliano hayo.
-
Marekani yaibua shaka kuhusu kufungamana kwake na JCPOA na kuondoa vikwazo
Apr 24, 2021 06:13Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika serikali ya Marekani alisema Alkhamisi kwamba hakuna dhamani ya kimaandishi itakayotolewa na serikali hiyo kuthibitisha kwamba haitajiondoa tena katika mapatano ya nyukilia na Iran na madola mengine makuu ya dunia, mashuhuri kama JCPOA.
-
Iran haitaruhusu mazungumzo ya Vienna kuhusu JCPOA yawe marefu kupita kiasi
Apr 21, 2021 03:02Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema Jamhuri ya Kiislamu haitamruhusu yeyote ayageuze mazungumzo ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanayofanyika huko Vienna, mji mkuu wa Austria kuwa marefu kupita kiasi na yasiyo na kikomo.
-
Iran: Kurutubisha urani kwa 60% ni jibu kwa njama za maadui
Apr 18, 2021 22:24Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema urutubishaji wa madini ya urani kwa kiwango cha asilimia 60 hapa nchini ni jibu kwa njama na chokochoko za maadui wa taifa hili.
-
Araqchi: Nchi za Ulaya zinapaswa kuonyesha zinayapa uzito mazungumzo ya nyuklia
Apr 16, 2021 03:22Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tume ya Pamoja ya Mapatano ya Nyuklia ya JCPOA ilifanya kikao chake Vienna, Austria jana Alhamisi ambapo kikao hicho kilikuwa na changamoto nyingi.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu mazungumzo ya nyuklia; sharti la Iran, msingi wa kuhuishwa JCPOA
Apr 15, 2021 23:05Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, siasa za Iran kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ziko wazi, na maafisa wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya kuhuishwa makubaliano hayo wanapaswa kuwa macho ili yasirefushwe kupita kiasi, suala ambalo lina madhara kwa taifa.
-
Sheikh Naim Qassim: Ushindi wa Iran ni ushindi wa mhimili wa muqawama
Apr 12, 2021 03:39Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, kuirejesha Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kutakuwa ni ushindi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.