Dec 16, 2020 07:47
Msemaji wa Wizara ya Mambo yaNje ya Iran Saeed Khatibzadeh ameeleza kuwa, Kikao cha Kamisheni ya Pamoja ya Mapatano ya JCPOA ni kati ya vikao vya kawaida vya kuchunguza mchakato wa utekelezaji wa mapatano ya JCPOA na masuala yanayozikwamisha pande nyingine husika za mapatano kutekeleza ahadi na majukumu yao.