Guterres ataka nchi wanachama wa UN kushirikiana na Iran kibiashara
(last modified Sat, 19 Dec 2020 12:19:52 GMT )
Dec 19, 2020 12:19 UTC
  • Guterres ataka nchi wanachama wa UN  kushirikiana na Iran kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza katika ripoti ya utekelezaji wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya udharua wa kulindwa mapatano ya JCPOA na kuzitaka nchi zote wanachama wa umoja huo kuanzisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na Iran kwa mujibu wa azimio hilo.

Antonio Guterres amesisitiza katika ripoti hiyo ya utekelezaji wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama kwamba nchi zote wanachama, taasisi za kieneo na za kimataifa zinaunga kutekelezwa mapatano ya JCPOA na kueleza kuwa, mpango huo ni njia bora kwa kuwa na matumaini na njia moja ya utatuzi wa pamoja, ya muda mrefu na inayofaa kwa ajili ya kadhia ya nyuklia ya Iran na pia kusaidia amani na usalama wa kieneo na kimataifa.  

Guterres aidha ameeleza kusikitishwa na hatua na uamuzi wa upande mmoja wa Marekani wa kujitoa katika mapatano ya JCPOA na kueleza kuwa, kuiwekea nchi nyingine vikwazo ambavyo vilikuwa vimeondolewa au kufutwa kwa mujibu wa mapatano hayo ni kinyume na malengo yaliyoainishwa ndani ya mapatano ya JCPOA na katika azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama. 

Baraza la Usalama lasisitiza kutekelezwa azimio nambari 2231 kuhusu JCPOA  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameshiria madai ya serikali ya Trump kwa ajili ya kustafidi na mfumo wa mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa au kuvirejesha vikwazo vyote vya Baraza la Usalama ambavyo vimemalizika kwa mujibu wa azimio hilo na kuongeza kuwa, akthari ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimetangaza katika barua kwa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama kwamba, barua ya Agosti 20 ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani haimaanishi kipengee cha 11 cha azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama.  

Ripoti hiyo imepangwa kusomwa Jumanne ijayo katika kikao cha kiduru cha Baraza la Usalama cha kujadili utekelezaji wa azimio hilo nambari 2231.  

 

Tags