Apr 05, 2019 13:16
Makubaliano ya nyuklia, yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) yanahesabiwa kuwa ni makubaliano muhimu sana kwa ajili ya kudumisha amani na usalama wa kimataifa; lakini Marekani imekuwa ikiyachimba kwa dhamira ya kuyasambaratisha, hasa kutokana na hatua iliyochukuliwa na nchi hiyo tarehe 8 Mei, 2018 ya kutangaza kujitoa kwenye makubaliano hayo ya kimataifa.