Zarif: Iran kamwe haitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani
(last modified Mon, 01 Apr 2019 03:11:24 GMT )
Apr 01, 2019 03:11 UTC
  • Zarif: Iran kamwe haitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua dhidi ya Iran zinazochukuliwa na Marekani na kusema: "Wairani kamwe hawatasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani."

Katika ujumbe aliouandika Jumapili katika ukurasa wake wa Twitter, Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisisitiza kuwa, sera za Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Iran zimefeli na kuongeza kuwa rais Trump anatumia chochote kilichofeli katika sera zake za Iran na kujaribu kuonyesha kuwa ni mafanikio.

Amesema kile alichosalia nacho rais wa Marekani ni kufurahia kuhusu kile anachodhani ni masaibu aliyowaletea watu wa Iran. Zarif ameendelea kusema kuwa, Trump, kama marais waliomtanguali wa Marekani, hatimaye atajifunza kuwa, Wairani kamwe hawawezi kusalim amri.

Ikumbukwe kuwa mnamo Mei 8 mwaka 2018, Rais Trump wa Marekani alichukua uamuzi wa upande moja na kukiuka ahadi za nchi yake kwa kujiondoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya Iran maarufu kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA).

Baada ya kujiondoa katika JCPOA, Marekani ilitangaza  kuiwekea Iran vikwazo ikiwa ni pamoja kuzuia uuzaji wa mafuuta ghafi ya petroli ya Iran nchi ya nchi.

Tags