-
Umoja wa Ulaya: Uungaji mkono wetu kwa makubaliano ya JCPOA uko pale pale
Oct 31, 2018 21:53Umoja wa Ulaya umejibu tuhuma za hivi karibuni za Denmark dhidi ya Iran kwa kusema: Brussels inasubiri taarifa zaidi kutoka Copenhagen kuhusu suala hilo na kwamba uungaji mkono wa umoja huo kwa makubaliano ya JCPOA uko pale pale.
-
Ulaya yakerwa na vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusisitiza kulindwa mapatano ya JCPOA
Oct 30, 2018 22:50Rais Donald Trump wa Marekani daima amekuwa akijaribu kuvuruga mapatano ya kimataifa yaliyofikiwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 kwa kisingizio kuwa ni mapatano mabaya zaidi ya kimataifa kuwahi kufikiwa na Marekani.
-
Ulaya na Umoja wa Mataifa zasisitiza azma yao ya kuyalinda makubaliano ya JCPOA
Oct 25, 2018 08:28Licha ya Marekani kuyapinga makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, lakini nchi za Ulaya zinasisitiza kulindwa makubaliano hayo muhimu ya kimataifa. Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akichukua misimamo iliyo dhidi ya makubaliano hayo ambayo yalifikiwa mwezi Julai mwaka 2015 kati ya Iran na kundi la 5+1 ikiwemo marekani yenyewe na anayataja kuwa ni makubaliano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa!
-
Uungaji mkono wa wakuu wa nchi za Asia na Ulaya kwa makubaliano ya JCPOA
Oct 20, 2018 08:31Japokuwa Marekani ni miongoni mwa nchi sita ambazo zilifikia makubaliano ya nyuklia na Iran katika kalibu ya nchi zinazounda kundi la 5+1 mwezi Januari mwaka 2015 lakini Rais Donald Trump wa nchi hiyo ameonekana akichukua msimamo wa kuyapinga makubaliano hayo; huku akiyataja kuwa ni makubaliano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa.
-
Uingereza: Kufungamana na JCPOA ni msingi wa uhusiano wetu na Iran
Oct 14, 2018 04:21Balozi wa Uingereza nchini Iran amesema kufungamana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kama mapatano ya kimataifa ni msingi wa uhusiano wa London na Tehran.
-
Sisitizo la Russia na India la kutekelezwa kikamilifu mapatano ya nyuklia ya JCPOA
Oct 07, 2018 23:03India na Russia wakiwa wanachama wa kundi la BRICS ambao wanataka mabadiliko katika muundo wa kimataifa utakao kuwa mbali na udhibiti wa Magharibi hususan Marekani, zimetangaza tena uungaji mkono wao kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
JCPOA, fursa kwa ajili ya kujitegemea kifedha Ulaya
Oct 06, 2018 22:56Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akikosoa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ambayo yalifikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 ikiwemo na Marekani yenyewe na kuyatataja makubaliano hayo kuwa ndiyo mabaya zaidi kuwahi kufikiwa.
-
Pigo jingine kubwa kwa Trump: Mahakama ya juu zaidi ya UN yaiamrisha Marekani iiondolee vikwazo Iran + Video
Oct 03, 2018 10:59Tehran imepata ushindi mwingine mbele ya Marekani baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kutoa amri kwa Washington kusimamisha vikwazo vyake vya upande mmoja haraka iwezekanavyo dhidi ya Iran.
-
Qassemi: Msimamo wa Ulaya unakidhi maslahi ya Iran katika JCPOA
Oct 01, 2018 11:17Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kumekuwa na hali ya kukaribiana misimamo ya Iran na Ulaya kuhusiana na kukidhiwa maslahi ya Tehran baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa kifupi.
-
Zarif: Ikiwa utaratibu uliowekwa na Ulaya hautotekelezeka, Iran itajitoa kwenye JCPOA
Sep 30, 2018 04:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, ikiwa utaratibu maalumu ulioratibiwa na Ulaya kwa ajili ya kuyalinda makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hautakuwa na ufanisi wa utekelezaji, Iran itajitoa kwenye makubaliano hayo.