Qassemi: Msimamo wa Ulaya unakidhi maslahi ya Iran katika JCPOA
(last modified Mon, 01 Oct 2018 14:47:46 GMT )
Oct 01, 2018 14:47 UTC
  • Qassemi: Msimamo wa Ulaya unakidhi maslahi ya Iran katika JCPOA

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kumekuwa na hali ya kukaribiana misimamo ya Iran na Ulaya kuhusiana na kukidhiwa maslahi ya Tehran baada ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa kifupi.

Bahram Qassemi amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari wa ndani na wa nje na kueleza kwamba kuna makubaliano kati ya Iran na Ulaya juu ya kuendeleza ushirikiano katika fremu ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba, baada ya mazungumzo na majadiliano ya muda mrefu kikiwemo kikao cha New York kati ya Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na kundi la 4+1, pande mbili hizo zimekubaliana kuuendeleza ushirikiano katika mazingira mapya.

Mkutano wa JCPOA Vienna, Austria

Qassemi amesema bayana kwamba, kutokana na mazingira maalumu yaliyosababishwa na Marekani ya kuyazuia mataifa mengine kushirikiana kiuchumi na Iran, mazungumzo kati ya Iran na Umoja wa Ulaya yameandaa mipango na mikakati ambayo itazingatia maslahi ya kitaifa.

Akizungumzia matamshi ya hivi karibuni ya Sergei Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba, nchi yake ipo tayari kuwa mpatanishi kati ya Iran na Israel, Bahram Qassemi amesema wazi kuwa, walimwengu wote wanatambua kwamba, msimamo wa Tehran kwa utawala haramu wa Israel ukoje. Ameongeza kuwa, Iran haiutambui rasmi utawala haramu wa Israel na katu haitakubali kuweko upatanishi kati yake na utawala huo ghasibu.

Tags