-
Mtifuano wa ana kwa ana kati ya Palestina na asasi za Waarabu kuhusu Makubaliano ya Abraham
Sep 09, 2020 09:06Kikao cha leo cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League kimefanyika wakati msimamo ulioonyeshwa na jumuiya hiyo pamoja na Baraza Kuu la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi GCC, hususan katika siku za karibuni kuhusu mapatano yaliyofikiwa kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni wa Israel umethibitisha kuwa, tajiriba ya uchukuaji maamuzi kitaasisi katika Ulimwengu wa Kiarabu imefeli;
-
Harakati ya PFLP yataka kutimuliwa Imarati katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
Sep 05, 2020 21:56Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) amesema kuwa, hatua ya Imarati ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel inakinzana na uamuzi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu hivyo ametoa wito wa kutimuliwa nchi hiyo sambamba na kurejeshwa Syria katika jumuiya hiyo.
-
Arab League yawaacha mkono Wapalestina na kuunga mkono mapatano ya UAE na Wazayuni
Sep 03, 2020 03:38Katika hatua inayoonyesha kuipiga vita na kuiacha mkono Palestina na badala yake kuunga mkono hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya kufanya mapatano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imelikataa ombi la Palestina la kuitishwa kikao cha dharura cha jumuiya hiyo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen: Arab League imepoteza mwelekeo
Aug 26, 2020 03:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) haina uwezo wa kulinda maslahi ya nchi za Kiarabu mbele ya njama mbalimbali zinaofanywa na utawala haramu wa Israel na washirika wake.
-
Algeria yakosoa misimamo ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusiana na Libya na Syria
Jul 12, 2020 23:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amekosoa misimamo ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusiana na Libya na Syria.
-
Tamim: Wakati umefika wa kuweka wazi uhusiano wa Israel na Waarabu
Jun 07, 2020 22:05Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi la Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu ameibua mijadala na wimbi la malalamiko baada ya kutoa mwito kwa nchi za Kiarabu kuufanya wa kawaida uhusiano wao na utawala haramu wa Israel.
-
Arab League yatahadharisha kuhusu hatua ya Israel ya kulitumia vibaya janga la Corona
Apr 08, 2020 03:33Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amezungumza kwa simu na Katibu wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) na kutahadharisha kuhusu hatua ya Israel ya kutumia vibaya janga la virusi vya corona.
-
Arab League yatahadharisha kuhusu hatari ya corona kwa wafungwa wa Kipalestina huko Israel
Apr 06, 2020 22:20Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetahadharisha kuhusu hatari kubwa inayotishia uhai wa wafungwa karibu elfu tano wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika korokoro za utawala haramu wa Israel kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.
-
Baada ya kushindwa kutatua mgogoro wa Libya, Arab League yasema inasikitishwa na mapigano wakati huu wa kushughulikia corona
Apr 04, 2020 22:22Baada ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kushindwa kutatua mgogoro wa Libya na kukomesha mapigano katika nchi hiyo ya Kiarabu ya kaskazini mwa Afrika, Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo ameishia kusema anasikitishwa na vita vinavyoendelea huko Libya badala ya kuelekezwa nguvu katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19.
-
Jumapili, Machi 22, 2020
Mar 21, 2020 22:02Leo ni Jumapili tarehe 27 Rajab mwaka 1441 Hijria, sawa na tarehe 22 Machi 2020 Miladia