-
Muqtada al-Sadr: Ubalozi na kambi zote za kijeshi za Marekani nchini Iraq zipigwe kufuli mara moja
Jan 05, 2020 16:26Muqtada al-Sadr, Kiongozi wa Harakati ya Al-Sadr ya nchini Iraq ametoa ujumbe leo kwenda kwa spika wa bunge akitaka kupigwa kufuli ubalozi wa Marekani na kambi zake za kijeshi nchini humo.
-
Nasrullah: Siku ya kuuawa shahidi Kamanda Soleimani, mwanzo wa historia mpya Mashariki ya Kati + Video
Jan 05, 2020 15:56Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Mwili wa shahidi Qassem Soleimani na ya mashahidi wenzake yasindikizwa na kuagwa Ahvaz na Mashhad + Video
Jan 05, 2020 15:40Mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kamanda wa kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na ya mashahidi wenzake waliouliwa shahidi pamoja naye katika jinai ya kinyama iliyofanywa na majeshi ya kigaidi ya Marekani imesindikizwa na kuagwa leo katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mwa Iran na huko Ahvaz kusini mwa nchi.
-
Sheikh Naim Qassem ahani msiba nyumbani kwa Kamanda Soleimani; asema mapambano yataendelea kwa nguvu zaidi
Jan 05, 2020 14:26Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema kuwa ni wazi kuwa njia na mstari wa mapambano utaendelea kwa nguvu zaidi kufuatia kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na wenzake aliokuwa amefuatana nao.
-
Ukosoaji wa Russia dhidi ya njama za Marekani za kubadili mlingano wa nguvu Asia Magharibi na kuongeza vitisho vya usalama kimataifa
Jan 05, 2020 13:21Hatua za Marekani katika eneo la Asia Magharibi hususan za kuzidisha uwepo wake kijeshi, mashinikizo dhidi ya Iran na hatimaye kutekeleza hatua za kigaidi hasa za kumuua shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la IRGC, Naibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Hashdu sh-Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes na shakhsia wengine walioambatana nao, zimekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa Russia kama mmoja wa wacheza karata muhimu katika eneo hili.
-
Rouhani: Marekani italipa gharama kubwa ya kumuua shahidi Soleimani
Jan 05, 2020 07:50Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Marekani itabeba dhima ya matokeo mabaya na radimali za kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi la Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) na kusisitiza kuwa, Washington italipa gharama kubwa ya ugaidi wake huo.
-
Pakistan yatoa radiamali kali kufuatia hujuma ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Qassem Soleimani
Jan 05, 2020 04:29Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan imesema kuwa, kitendo cha kigaidi kilichofanywa na Marekani cha kumuua shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, kitasababisha ukosefu wa amani katika eneo.
-
Maelfu ya Waislamu nchini India waandamana kulaani kuuliwa shahidi Qassem Soleimani
Jan 05, 2020 04:29Maelfu ya Waislamu nchini India wamelaani vikali kitendo cha Marekani cha kumuua kigaidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC.
-
Taathira za kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandis
Jan 05, 2020 04:28Usiku wa manane wa kuamkia juzi Ijumaa Januari 3 viongozi wa Marekani walitekeleza kitendo cha kijinai na kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kujitolea wa Iraq (Hashdu al Shaabi).
-
Mwili mtoharifu wa Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani wawasili Iran ya Kiislamu
Jan 05, 2020 05:06Mwili mtoharifu wa Shahidi Luteni Jenerali Haj Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) umewasili katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo asubuhi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Ahwaz kusini mwa nchi.