-
Usalama waimarishwa Kenya, wananchi wanasubiri uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kura za uchaguzi wa Septemba 9
Sep 05, 2022 02:41Usalama umeirishwa katika maeneo mbalimbali ya Kenya hususan katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, huku Wakenya wakisubiri kwa hamu na ghamu uamuzi unaotarajiwa kutolewa leo na Mahakama ya Juu ya nchi hiyo kuhusu shauri lililowasilishwa mahakamani na mgombea urais wa chama cha Muungano wa Azimio la Umoja wa One Kenya, Raila Odinga akipinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 9 mwezi uliopita.
-
Majaji wa Afrika wawasili Kenya kufuatilia kesi ya uchaguzi wa rais
Aug 29, 2022 06:41Wanachama wa Jumuiya ya Majaji na Mahakimu wa Afrika wamewasili jijini Nairobi, kufuatilia shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) hivi karibuni.
-
Wakenya waishitaki Uingereza kwa jinai za enzi za ukoloni
Aug 24, 2022 06:25Kundi la raia wa Kenya limeifungulia mashitaka serikali ya Uingereza katika Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya, likitaka iwajibishwe kwa jinai ilizotenda dhidi ya wananchi wa Kenya enzi za ukoloni.
-
Odinga aenda mahakamani kupinga matokeo ya urais Kenya
Aug 22, 2022 06:48Mgombea urais wa Kenya kwa tiketi ya chama cha Muungano wa Azimio la Umoja wa One Kenya, Raila Odinga amewasilisha mahakamani shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC hivi karibuni.
-
Iran yatoa pongezi kufuatia kufanyika uchaguzi wenye mafanikio Kenya
Aug 19, 2022 23:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza wananchi na serikali ya Kenya kwa kufanyika kwa mafanakio uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
-
Mgombea urais wa Azimio Kenya apinga matokeo yaliyomtangaza Ruto mshindi
Aug 16, 2022 09:57Raila Odinga, mgombea urais wa Kenya kwa tiketi ya Muungano wa Azimio amesema hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kwa sababu mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alikiuka katiba kabla ya kumtangaza mshindi.
-
Marais, viongozi wa kieneo wampongeza Rais mteule wa Kenya, William Ruto
Aug 16, 2022 03:34Marais a viongozi wa nchi kadhaa za Afrika wamemnyooshea mkono wa pongezi William Ruto kwa kuibuka mshindi katika uchaguzi wa kiti cha rais nchini Kenya uliofanyika wiki iliyopita.
-
Wakenya wasubiri muelekeo wa Odinga baada ya Ruto kutangazwa mshindi wa urais
Aug 15, 2022 23:10Wananchi wa Kenya hususan wafuasi wa mwanasiasa mkongwe Raila Odinga wanasubiri tangazo na muelekeo utakaochukuliwa na mgombea huyo wa kiti cha rais kupitia chama cha Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya katika uchaguzi wa Jumanne iliyopita, baada ya mshindani wake William Ruto wa chama cha UDA kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo.
-
Mwito wa amani watolewa huku Wakenya wakiendelea kusubiri matokeo ya urais
Aug 14, 2022 23:44Viongozi wa kidini na wakuu wa asasi za kiraia wametoa mwito kwa wananchi wa Kenya kuendelea kudumisha amani na kuwa watulivu huku wakisuburi matokeo ya uchaguzi wa rais.
-
Tume ya Uchaguzi Kenya yakanusha madai ya kudukuliwa mfumo wake
Aug 12, 2022 10:09Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) imepuuzilia mbali madai kuwa mfumo wake wa kuendesha uchaguzi umedukuliwa, huku Wakenya wakiendelea kusubiri kwa hamu na shauku kuu matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa rais.