-
Rais wa Kenya ataka uchaguzi ufanyike kwa amani kesho, kiongozi wa upinzani Raila Odinga aususia rasmi
Oct 25, 2017 13:07Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amelihutubia taifa jioni hii na kutoa mwito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio wa Rais na kuhakikisha usalama na amani inadumishwa nchini humo.
-
Mahakama ya Juu Kenya yaakhirisha kesi ya uchaguzi wa marudio kwa ukosefu wa akidi
Oct 25, 2017 04:45Kesi iliyowasilishwa katika Mahakama ya Juu na watetezi na wanaharakati wa haki za binadamu ya kutaka kuakhirishwa uchaguzi wa rais wa marudio nchini Kenya imekosa kufanyika kutokana na ukosefu wa akidi.
-
Odinga: Wafuasi wetu wasiandamane siku ya uchaguzi wa marudio
Oct 24, 2017 11:35Kinara wa muungano wa upinzani NASA nchini Kenya amewataka wafuasi wa mrengo huo kutofanya maandamano wakati wa uchaguzi wa marudio wa urais unaotazamiwa kufanyika Alkhamisi wiki hii.
-
SAUTI: Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya lawachagua viongozi wapya, watakiwa kutatua matatizo ya Waislamu
Oct 23, 2017 13:20Hatimaye Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya limefanya uchaguzi wa ndani ikiwa ni baada ya kupita zaidi ya miaka 10.
-
UN na AU zatoa wito wa amani kabla ya uchaguzi wa marudio Kenya
Oct 23, 2017 10:24Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zimetoa taarifa ya pamoja zikitoa wito kwa wanasiasa na polisi nchini Kenya kuzingatia sheria katika kutatua mgogoro uliopo nchini humo.
-
Helikopta yaanguka Kenya, wanachama wa Jubilee wanaaminika kuaga dunia
Oct 21, 2017 13:31Ndege moja aina ya helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.
-
Polisi Kenya: Watu 4 wameuawa katika maandamano ya upinzani
Oct 20, 2017 13:43Polisi ya kenya imesema kuwa watu wanne wameuawa katika maandamano ya upinzani nchini humo katika kipindi cha wiki mbili zilizopita huku uchaguzi wa rais wa marudio ukikaribia kufanyika wiki ijayo. Polisi ya Kenya imesema kuwa watu hao waliuawa katika mapigano yaliyotokea kati ya maafisa polisi na waandamanaji.
-
Chama cha Jubilee chawashitaki viongozi wa NASA kwa kuwashawishi Wakenya kususia uchaguzi
Oct 20, 2017 01:13Katibu Mkuu wa Chama cha Jubelee nchini Kenya, Raphael Tuju amesema kuwa uongozi wa chama hicho umewasilisha kesi katika Mahakama ya Juu ambayo iliagiza uchaguzi wa urais urudiwe.
-
Mmoja wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ya IEBC nchini Kenya ajiuzulu
Oct 18, 2017 11:48Mmoja kati ya viongozi wanane wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) nchini Kenya ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo mapema leo Jumatano.
-
Upinzani Kenya wasimamisha maandamano, Ruto amtaka Odinga ashiriki uchaguzi
Oct 17, 2017 11:57Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umetangaza kusimamisha maandamano ya kushinikiza marekebisho kwenye Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuelekea uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.