-
Ripoti ya siri ya UN: Korea Kaskazini inajizatiti kulinda nguvu zake za makombora na silaha za nyuklia
Feb 05, 2019 15:50Ripoti ya siri iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, Korea Kaskazini inaendeleza shughuli zake za kijeshi za kulinda nguvu na uwezo wake wa makombora na silaha za nyuklia ili kuhakikisha haziwezi kuangamizwa kwa mashambulio ya kijeshi.
-
Korea Kaskazini yalaani vikali uingiliaji wa Marekani nchini Venezuela
Feb 04, 2019 13:55Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imetoa taarifa inayolaani uungaji mkono wa nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kwa Juan Gerardo Guaidó kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa muda wa Venezuela na uingiliaji wa nchi hizo katika nchi hiyo na kusema kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa kuchupa mipaka wa sheria za kimataifa.
-
Korea Kusini: Korea Kaskazini inatakiwa kuharibu kikamilifu kituo kikuu cha silaha zake za nyuklia
Jan 25, 2019 08:08Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini amesema kuwa, ili kudhibiti miradi yake ya nyuklia hususan wakati wa kujiri mkutano wa viongozi wa Washington na Pyongyang, Korea Kaskazini inatakiwa kuharibu kabisa kituo kikuu cha silaha zake za nyuklia na kadhalika iruhusu wakaguzi wa kimataifa kufika eneo hilo kwa ajili ya kuthibitisha suala hilo.
-
Muda wa kikao cha pili kati ya Trump na Kim Jong-un watangazwa
Jan 19, 2019 08:06Shirika la Habari la Korea Kusini, Yonhap limetangaza muda utakaofanyika kikao cha pili kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini kwamba itakuwa mwishoni mwa mwezi ujao.
-
Russia yakanusha madai ya Marekani kwamba imeipatia Korea Kaskazini teknolojia ya makombora
Jan 18, 2019 15:38Balozi wa Russia nchini Korea Kaskazini amekanusha tuhuma za viongozi wa Marekani dhidi ya nchi yake kwamba Moscow imeipatia Pyongyang teknolojia ya makombora na kuongeza kwamba, tuhuma hizo ni za kuudhi kama ambavyo hazina msingi wowote.
-
Rais Moon Jae-in: Kikao cha pili cha Trump na Kim Jong-un kitafanyika karibuni hivi
Jan 11, 2019 01:11Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amesema kuwa, kikao cha pili cha viongozi wa Marekani na Korea Kaskazini na pia safari ya Kim Jong-un mjini Seoul, itafanyika hivi karibuni.
-
Trump: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini vitaendelea kutekelezwa
Jan 07, 2019 04:29Rais Donald Trump wa Marekani amesisitiza juu ya kuendelea kutekelezwa kikamilifu vikwazo vya nchi yake dhidi ya Korea Kaskazini na amesema kuwa, vikwazo hivyo vitaendelea kuwepo.
-
Marekani yaendelea kuisakama Korea Kaskazini, yamuwekea vikwazo anayeisaidia kununua mafuta
Nov 20, 2018 15:17Katika mwendelezo wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini, Wizara ya Fedha ya nchi hiyo imemuwekea vikwazo mfanyabiashara mmoja wa Russia kwa tuhuma za kuidhaminia mafuta Pyongyang.
-
Korea Kaskazini yafanyia majaribio silaha mpya na ya kisasa chini ya usimamizi wa Kim Jong-un
Nov 16, 2018 04:24Serikali ya Korea Kaskazini imefanyia majaribio kwa mafanikio, ya silaha ya 'kistratijia, mpya na ya kisasa' chini ya usimamizi wa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.
-
Korea Kusini yakadhibisha ripoti ya taasisi ya kifikra ya Marekani kuhusu Korea Kaskazini
Nov 13, 2018 14:43Ofisi ya Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini imekadhibisha ripoti ya taasisi ya kifikra ya Marekani ya 'Kituo cha Utafiti wa Kimataifa na Kistratijia' juu ya kuendelea shughuli za makombora ya siri ya Korea Kaskazini.