Korea Kaskazini yalaani vikali uingiliaji wa Marekani nchini Venezuela
(last modified Mon, 04 Feb 2019 13:55:28 GMT )
Feb 04, 2019 13:55 UTC
  • Korea Kaskazini yalaani vikali uingiliaji wa Marekani nchini Venezuela

Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imetoa taarifa inayolaani uungaji mkono wa nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani kwa Juan Gerardo Guaidó kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa muda wa Venezuela na uingiliaji wa nchi hizo katika nchi hiyo na kusema kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa kuchupa mipaka wa sheria za kimataifa.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo sambamba na kukosoa hatua ya Marekani ya kuingilia masuala ya ndani ya Venezuela imemtaja Rais Nicolás Maduro kuwa rais halali wa nchi hiyo na aliyechaguliwa kwa mujibu wa katiba. Kadhalika Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imebainisha kwamba suala la Venezuela lazima litatuliwe kwa njia za amani na kwa mujibu wa maamuzi ya serikali na watu wa nchi hiyo tu. Hii ni katika hali ambayo Marekani na washirika wake zinafanya juu chini kutekeleza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Rais Maduro kupitia kumuunga mkono Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani wa nchi hiyo.

Korea Kaskazini yenye uhusiano mwema na serikali ya Venezuela

Katika uwanja huo tarehe 23 Januari Guaidó alichukua hatua ambayo ilitajwa na serikali na watu wa Venezuela kuwa mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Nicolás Maduro aliyechaguliwa na wananchi, baada ya mpinzani huyo kujitangaza kuwa rais wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo akthari ya nchi ikiwemo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, China, Cuba, Uturuki, Afrika Kusini, Uruguay na Italia zimelaani vikali uingiliaji wa Marekani na nchi za Magharibi ndani ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini sambamba na kutangaza uungaji mkono wao kwa Rais Maduro.

Tags