Waziri wa Ulinzi wa Pakistan: US ilipaswa kumteka Netanyahu, si Maduro
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan amesema "Marekani inapaswa kumteka nyara na kumshtaki katika mahakama yake yoyote ile Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu, ikiwa Washington ni rafiki halisi wa ubinadamu."
Waziri wa Ulinzi wa Pakistani Khawaja Asif ameeleza amesema hayo katika mahojiano na televisheni ya nchi hiyo na kueleza kuwa, "Washington inapaswa kuliamuru jeshi lake kumkamata Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na "kumshtaki katika mahakama yake yoyote,kwani Netanyahu ndiye "mhalifu mbaya zaidi wa ubinadamu duniani."
Asif amelaani operesheni ya Marekani nchini Venezuela na kuelezea kukamatwa kwa Rais Nicolas Maduro kuwa ni utekaji nyara, akisitiza kuwa hatua hiyo ingelikuwa ya haki tu iwapo ingelitekelezwa dhidi ya Israel.
Baada ya uvamizi huo wiki moja iliyopita, serikali ya Marekani ilimshtaki Maduro kwa ulanguzi wa mihadarati, tuhuma ambazo amekuwa akikanusha mara kwa mara, ikisema hatua za Washington zinalenga kunyakua maliasili ya nchi yake hasa mafuta.
"Hatua za Marekani "zilifungua kisanduku cha Pandora" kwa kuhalalisha mbinu ambayo "ilikuwa na utata mkubwa" hapo awali, Asif ameiambia kanali ya Geo TV wa Pakistan katika mahojiano ya karibuni. "Niadhamu ya ulimwengu inaporomoka," Waziri wa Ulinzi wa Pakistan ameonya, akiongeza kwamba kile ambacho Washington ilikifanya "si kitu kizuri cha kufanya."
Watu zaidi ya 200 waliuawa na kujeruhiwa wakati wa kutekwa Maduro katika operesheni ya kivamizi iliyofanywa na jeshi la Marekani kwa amri ya Rais Donald Trump mnamo Januari 3.
Jamii ya kimataifa imeendelea kulaani hatua hiyo ya wanajeshi wa Marekani ya kumteka nyara Maduro na mkewe Cilia Flores na kuwasafirisha hadi Marekani kwa ajili ya kushtakiwa kwa madai ya kubambikiwa ya magendo ya mihadarati, kula njama, kuingiza kokaini nchini Marekani na magendo ya silaha.