Rais wa muda: Venezuela ina haki ya kujenga uhusiano na Iran
-
Delcy Rodriguez
Rais wa uongozi wa muda wa Venezuela, Delcy Rodriguez, amethibitisha tena kwamba Caracas ina haki ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na China, Cuba, Iran na Russia na kupinga uingiliaji wa Marekani. Rais wa serekali muda ya Venezuela pia amekosoa hatua za kichokozi za Washington dhidi ya nchi hiyo.
Bi Delcy Rodriguez amesisitiza kuwa Venezuela ina haki ya kuratibu na kupanga sera yake ya kigeni. "Tuna haki za kuwa na uhusiano wa kidiplomasia na China, Russia, Iran na Cuba na pia na watu wote duniani; sisi ni nchi yenye mamalaka ya kitaifa," amesema Rais wa uongozi wa muda wa Venezuela.
Rodriguez amelaani chokokocho za uvamizi wa Marekani Januari 3 mwaka huu na kuzitaja chokochoko hizo kuwa doa katika uhusiano wa nchi mbili.
Amesisitiza kuwa, serikali yake imeamua kuchagua njia ya diplomasia kukabiliana na mgogoro iliotishwa Venezuela licha ya hatua za uhasama za Washington.
Akielezea wakati wa sasa kuwa ni mwanzo wa "zama mpya ya kisiasa," Rodriguez ametumia sehemu kubwa ya hotuba yake kwa kumuenzi Rais Nicolas Maduro na mkewe, Cilia Flores, ambao walitekwa nyara wakati wa mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Caracas tarehe 3 mwezi huu.
Rais wa muda wa Venezuela ameahidi kuendeleza jitihada za kuhakikkisha kwamba Maduro na mkewe wanaachiliwa huru.