-
Wapalestina 1373 wauawa shahidi wakisubiri msaada wa chakula Gaza
Aug 03, 2025 02:37Ofisi ya Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa: Tokea tarehe 27 Mei mwaka huu hadi sasa Wapalestina 1373 wameuliwa shahidi katika Ukanda wa Gaza wakati walipokuwa wakisubiri kugawiwa msaada wa chakula. Waliuliwa shahidi kwa kufyatiliwa risasi na wanajeshi wa Kizayuni.
-
Wapalestina waliouliwa shahidi na jeshi la kizayuni Ghaza wakaribia 60,000; 92 wauawa kwa siku moja
Jul 29, 2025 07:01Idadi ya Wapalestina waliouwa shahidi kwa mashambulizi ya kinyama ya jeshi la utawala wa kizayuni katika Ukanda wa Ghaza inakaribia 60,000 baada ya jeshi hilo katili kuwaua Wapalestina wengine 92 katika muda wa siku moja wakiwemo 41 waliokuwa wakihangaika kupata msaada wa chakula.
-
Makumi ya wafanyakazi wa huduma za uokoaji na raia wauawa shahidi katika mashambulizi mtawalia ya Israel huko Gaza
Jul 03, 2025 04:01Duru za kitiba na za ndani ya Ukanda wa Gaza zimetangaza kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni jana alasiri lilitekeleza mashambulizi mapya katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu ambapo wakimbizi wa Kipalestina walikuwa wamepata hifadhi na kuuwa makumi ya watu.
-
Hilali Nyekundu ya Palestina: Ripoti ya Israel ya mauaji ya wahudumu wa tiba 'imejaa uwongo'
Apr 21, 2025 07:15Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina limekanusha vikali ripoti ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu mauaji liliyofanya mwezi uliopita ya zaidi ya wafanyakazi 15 wahudumu wa sekta ya tiba huko Ghaza, ambayo utawala huo umedai waliuawa kimakosa.
-
Israel yashambulia nyumba ya makazi ya raia huko Gaza na kuuwa shahidi watu 15
Apr 03, 2025 11:37Idadi nyingine ya Wapalestina wameuawa shahidi katika mashambulizi ya anga ya leo asubuhi utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
-
Kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake: Zaidi ya wanawake 12,000 wa Kipalestina wameuawa katika vita vya Gaza
Mar 08, 2025 12:54Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa: Wanawake 12,316 wa Kipalestina wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni Israel dhidi ya watu wa Gaza.
-
Watoto wachanga watano wafariki Ghaza kutokana na mgando wa baridi kali
Feb 25, 2025 10:59Watoto wachanga watano wamefariki dunia katika Ukanda wa Ghaza kutokana na mgando wa baridi kali katika eneo hilo lililowekewa mzingiro na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuzuiwa kuingizwa misaada ya kibinadamu ikiwemo ya vifaa vya huduma za tiba.
-
Kiongozi wa Mapinduzi atoa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Mahakimu wawili wa Idara ya Mahakama
Jan 19, 2025 10:41Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa salamu za rambirambi na mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi katika shambulio la kigaidi mahakimu wawili wa Idara ya Mahakama ya Iran.
-
Kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Qassem Soleimani
Jan 03, 2025 11:51Shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimanim aliuawa tarehe 3 Januari 2020 kwa ndege ya kivita ya jeshi la kigaidi la Marekani akiwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko rasmi wa waziri mkuu wa nchji hiyo. ****
-
Jeshi la Kizayuni lamuua Babu mtu wa Kipalestina aliyegusa nyoyo za walimwengu mitandaoni
Dec 17, 2024 06:05Shambulio la kinyama la makombora lililofanywa na jeshi la Kizayauni katika Ukanda wa Ghaza limemuua Khaled Nabhan, Mpalestina ambaye amefahamika sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na video iliyomuonyesha akibusu macho ya mjukuu wake aliyeuliwa na kumwita "roho ya roho yangu".