Sep 02, 2018 05:56
Ushindi mkubwa linaoendelea kuupata jeshi la Syria na waitifaki wake katika maeneo tofauti ya nchi hiyo, na hatua ya jeshi hilo ya kujiandaa hivi sasa kuusafisha mkoa wa Idlib kutokana na uchafu wa magenge ya kigaidi, imewatia kiwewe waungaji mkono wa magaidi hao yaani nchi za Magharibi na hasa Marekani. Mkoa wa Idlib ndiyo ngome ya mwisho wa magenge ya kigaidi nchini Syria.